Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka wakandarasi walioingia mkataba wa ujenzi wa miradi ya barabara kutekeleza kazi hizo kulingana na makubaliano na masharti yanavyoagiza ilikujiwekea heshima kwa serikali na jamii kwa ujumla
"Niwaombe mmeomba kazi mmepata kazi fanyeni kazi kwa mujibu wa mikataba mliyoipata leo mkifanya kazi vizuri itawasaidia kupata kazi nyingine ujenzi uanze mara moja kama mikataba inavyoeleza.
Ameyasema hayo leo septemba 8, 2022 mara baada ya halfa ya kusaini mikataba 40 ya matengenezo ya barabra ya mwaka wa fedha 2022/2023 TARURA Mkoa wa Pwani yenye dhamani ya Shilingi bilioni 10.8,
Aidha Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani leopold Lunji amesema fedha hizo zitakwenda kuongeza matengenezo ya barabara za lami kutoka kilometa 74 zilizopo hivi Sasa hadi kufikia kilometa 84, kufanya ukarabati kwa kiwango Cha changarawe kilometa 198, ujenzi wa makaravati 162 pamoja na ujenzi wa madaraja 8.
Mhe. Kunenge ametoa shukrani kwa uongozi wa awamu ya sita wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuupatia Mkoa wa Pwani fedha kwaajili ya miradi ya barabara na kuwahasa wakandarasi wawe waaminifu kulingana na mikataba hiyo.
Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu Mkoa waPwani huku ikishuhudiwa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani zuwena Omary.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.