• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RC kunenge awataka Wakulima Pwani kuhakikisha wanalima kwa tija na Kisasa.

Posted on: October 5th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge amewaasa wakulima wa zao la Korosho ,kuhakikisha wanalima kwa tija na kisasa ili kupata korosho zenye ubora na kujiongezea kipato

Aidha ametoa rai kwa wataalamu wa kilimo kuwa na mkakati utakaoweza kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.

Kunenge alitoa rai hiyo Oktoba 5, wakati akifungua mkutano wa wadau wa korosho mkoa wa Pwani ,uliofanyika katika Ukumbi wa Flex Garden Wilayani Mkuranga.

Aliwataka wakulima hao kuhakikisha wanajifunza kupitia kwa wenzao wa sehemu nyingine ili kuhakikisha wanaleta tija katika zao hilo.

"Kujifunza sio kosa , hivi kunashida gani tukapata mkulima mmoja anaefanya vizuri aje hapa tukajifunza kupitia yeye ili tuweze kufikia malengo na kufanya kilimo chenye tija."

"Ni matarajio yangu ifike mahala nikiambiwa eneo fulani wanazalisha korosho ,tija tunaona bado mkorosho mmoja unazalisha wastani wa kg 20,Tunadhani waingie wataalamu waangalie changamoto ni nini kama aidha aina ya miche aliyopanda ama afya ya udongo au ni madawa"

"Bila kufanya hivyo tutakuwa tunapiga kelele bure wakati mkoa wetu tunauendesha kitaalamu" alisema Kunenge.

Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani anaelekeza kuwa kama mfumo huo unatija ,iangaliwe namna ya mazao mengine ya biashara yaingie katika mfumo huo.

"Dunia ya leo hakuna mwananchi atakaekataa kitu kinachompa tija na maslahi ,wakulima hawa wanataka kubadili maisha yao kama kitu ni kizuri na kina maslahi mazuri kwake hawezi kukataa " alieleza Kunenge.

Vilevile aliwataka watendaji kuhakikisha wanasajili wakulima wote ili kuhakikisha wanapata pembejeo.

Pia Kunenge aliviasa Vyama vya Ushirika vinavyosimamia mazao hayo kuhakikisha wanasimamia bei nzuri ya mazao hayo ili kuhakikisha wakulima wanapata faida.

Akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji na uuzaji wa Korosho na Ufuta kwa mwaka 2022/2023 ,Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika (CORECU ) ,alisema Chama kwa kushirikiana na Sekretariet ya Mkoa kiliendesha jumla ya minada 9 ya Korosha ambapo vyama vya msingi 75 vilihusika katika kukusanya na uuzaji wa Korosho.

Anasema Jumla ya tan 12,151.339 ambapo tani 10,759.449 ziliuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na tani 1,391.840 ziliuzwa kwa wabanguaji wa ndani kupitia soko la awali chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Alieleza ,Bei ya juu ya wastan kwa korosho za daraja la kwanza ilikuwa ni sh. 1,892.92 na bei ya chini ya wastani daraja hilo ilikuwa ni sh.1,421.00 na daraja la pili ziliuzwa kwa bei ya juu wastani ya sh.1,520.00 na bei ya wastani ilikuwa sh. 1,202.02.

Alieleza ,thamani ya mauzo yote kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ni sh.Biln 18,789,041,912.

Anasema ,ubora wa korosho umeongezeka kutoka asilimia 72 msimu 2021/2022 na kufikia asikimia 96.3 msimu 2022/2023 .

Alibainisha kwamba, kati ya kilo 10,759,499 zilikusanywa ghalani na kilo 10,361,124 sawa na asilimia 96.3 ni daraja la kwanza na kilo 398,375 sawa na asilimia 3.7 ni daraja la pili.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.