Mkuu wa mkoa wa Pwani the. Abubakari Kunenge, amewataka wanananchi ambao wamevamia na kuweka kambi za uvuvi katika kisiwa cha Nyororo kilichopo katika wilaya ya Mafia kutekeleza mara moja agizo la serikali linalowataka kuhama mara moja katika kisiwa hicho ambacho ni eneo tengefu kwa ajili ya mazalia ya samaki katika bahari ya Hindi.
Kunenge ametoa rai hiyo Leo May 28,2022 wakati alipofanya ziara ya Kikazi katika kisiwa hicho kukutana na wananchi hao ambao wamevamia kisiwa hicho hakina huduma za kijamii na kuanzisha makambi ya kudumu.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, serikali kupitia kwa waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki tayari imeshakutana na wananchi hao na kuwataka waondoke katika eneo hilo mara moja lakini bado wameendelea kuwa wakaidi na jambo ambalo limemlazimisha katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo mengine kwa uongozi wa mkoa akiutaka uongozi huo usimamie agizo la kuondolewa kwa watu hao.
Amewataka wananchi hao kuheshimu agizo hilo kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na hakuna mtu yoyote aliyeko juu ya sheria,
Pia amewataka wananchi hao kupitia kwa mwenyekiti hao Said likuwawA kuunda kamati ya watu watano wafike ofisini kwake ili kujadiliana na namna ambavyo wataweza kumaliza tatizo hilo kwakuwa serikali serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani ni sikuvu na inawajali wananchi wake.
Kwa upande baadhi ya wakazi hao wameiomba serilali kuhalalisha kisiwa hicho kuwa makazi ya watu na kuanzisha kitongopji ndani ya kisiwa hicho ili wananchi waweze kupata huduma za kijamii .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.