Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge amezindua mbio za Wakala wa Barabara (TANROADS) Coast City Marathon ambayo inalenga kuhamasisha masuala ya Uwekezaji na viwanda Mkoani humo.
Kilele cha mbio hizo kinatarajiwa kufanyika Novemba 12 mwaka huu.
Akizungumza na wadau mbalimbali pamoja na wadhamini wa mbio hizo Wakala wa hifadhi za Misitu, NMB, ,NSSF wakiwemo wadhamini wakuu TANROADS , Kunenge alieleza michezo ni suala muhimu katika kujenga afya na ameahidi nae kushiriki kukimbia kilometa 21.
Aidha alieleza ,mkoa huo ni ukanda wa viwanda hivyo kupitia mbio hizo utaongeza wigo wa kujitangaza na kufungua milango kwenye sekta ya uwekezaji.
"Mkoa wetu kwasasa una viwanda 1,460 kati ya hivyo vikubwa 90 ambapo vya kati ni 138, tunahakikisha kuboresha miundombinu mizuri na kuweka Mazingira Bora ya uwekezaji kwa ajili ya kuwavutia kwa kasi"
Pia RC Kunenge aliwakaribisha wawekezaji, wafanyabiashara na wananchi kwenye maonyesho ya viwanda na biashara yanayotarajia kufanyika octoba 5-10 mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.