Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ameagiza kuchukuliwa hatua wale wote wanaobainika kusababisha hasara kwenye hoja za ukaguzi wa mahesabu na kuhakikisha hoja zote ambazo hazijafungwa zifungwe ifikapo Septemba 30 mwaka huu.
Vilevile ameagiza Halmashauri Mkoani hapo ,kuweka vipaombele ,kufungua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na Kuwa wabunifu ili kukuza uchumi na kuongeza uwezo wa Halmashauri .
Akizungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Kibaha , wakati wa Kikao Maalumu cha Kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,Kunenge aliwaasa watendaji kujenga tabia ya kuhifadhi na kutunza nyaraka ili kuepusha hoja ambazo zipo ndani ya uwezo wa kuzifunga.
Alionya kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kupuuzia mambo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha hatua za ukaguzi kukwama.
Kuhusu mabadiliko ya kiuchumi mkoa , Mkuu huyo wa mkoa alisema ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kasi za ufanyaji kazi ili kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi.
"Watendaji na wataalamu muwe wabunifu unaoendana na spidi ya Serikali na Rais Samia Suluhu kuleta matokeo chanya kwa wananchi," mkoa bado unahitaji nguvu ya pamoja kuinua uchumi,'"! ambao bado kimkoa haupo vizuri kwani Hadi Sasa mkoa upo mkoa wa tatu kutoka mwisho"alifafanua Kunenge.
Kunenge aliziasa, Halmashauri hizo, kumaliza miradi yote viporo ,kuweka Mazingira Bora ya kuvutia wawekezaji pamoja na kutangaza fursa mkoa.
Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoani Pwani ,Mary Dibogo alibainisha , wanaendelea na hoja nyingine za nyuma , wanashindwa kufunga baadhi ya hoja kutokana na Kuwa hawaoni namna ya kuzifunga .
Alitoa Rai Halmashauri zote ambazo bado Kuna hoja hazijafungwa ,wafunge hoja zilizobaki kwa muda waliopewa .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mshamu Munde alieleza , Halmashauri hiyo imepata hati safi mwaka wa tatu mfululizo na kueleza hoja zilikuwa 50 ,zilizofungwa 31 ,bado 19 hazijafungwa .
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Butamo Ndalahwa alielezea wamepata hati safi ,hoja 37 zimefungwa ," 26 hazijafungwa kati ya hizo 18 zipo nje ya uwezo wao kuzifunga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.