Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge amezitaka Halmashauri na Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaongeza mapato pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuinua uchumi wa Mkoa.
Aidha ameyataka mabaraza ya madiwani kuzungumza uchumi na fursa zilizopo ili kwenda na kipaombele cha kuinua uchumi .
Akizungumza katika kikao Cha Ushauri Cha mkoa (RCC) Kunenge alieleza ,wote kwa umoja wazungumzie mapato ili kupunguza kukopa, kwani mkoa huo ni wa viwanda haiwezekani kuona unashuka kiuchumi.
"Halmashauri ziongeze mapato, tuende pamojaa na uwezo wa kiuchumi, na niseme hapo nikizungumzia mapato sio halmashauri tuu na Taasisi zetu za Serikali zihakikishe zinaongeza mapato,hata Kama mnakusanya ,mtuambie mnakisanya kiasi gani na malengo yenu ni yapi"alifafanua Kunenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.