Mkuu wa Mko wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge leo Agost 8, 2022 amekutana na uongozi wa shirika la Maendelo la Taifa - NDC kwa mazungumzo ya kuitangaza Kongani ya Viwanda inayomilikiwa na Shirika hilo iliyopo Mjini Kibaha.
Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mhe. Kunenge amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Nicolaus Shombe kuhakikisha ofisi yake inaandaa mchoro wa eneo hilo kwa ajili ya kulitangaza na kuwaleta wawekezaji.
“Ni wajibu wangu kuzisemea taasisi zote zilizopo mkoani kwangu, hivyo mnapaswa kuandaa mchoro wa eneo hilo, mnipatie ili tuweze kulitangaza kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya uwekezaji,” alisema RC Kunenge.
Akifafanua faida za uwekezaji, Kunenge ameeleza kuwa unasaidia katika kufanisha malengo ya mkakati mkubwa wa mkoa wa kuongeza vyanzo vya mapato, hivyo eneo hilo la NDC ni muhimu na litasaidia kuongeza mapato kama atalisemea vizuri na likapata wawekezaji.
Katika Hatua nyingine RC Kunenge amewapongeza watendaji wote wa Sekretarieti ya Mkoa na wa Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwa utendaji wa kazi na kupelekea mkoa kushika nafasi ya tatu nchini kwa kigezo cha makusanyo mengi ki asilimia yanayotokana na mapato ya ndani.
Nae Mkurugenzi mtenda Wa shirika la Maendeleo ya Taifa NDC Dr. Nicolaus Shombe amemshukuru mkuu wa Mkoa huo kwa kuweza kukutana nao na kufanya mazungumzo ya kuendeleza eneo hilo.
Dr. Nicolas alifafanua kuwa Kongane la Viwanda TAMCO, Kibaha lina eneo ukubwa wa ekari 201.63 na limeteuliwa kujenga Viwanda katika Makundi matatu aliyoyataja kuwa ni Viwanda vya madawa na vifaa tiba, viwanda vya kuunganisha magari na mitambo pamoja na viwanda vya nguo.
Alisema eneo hilo linahitaji miundombinu ya barabara kama kilomita 4.8 na tayari Kilomita 1.6 imeshajengwa.
Dr. Pia alieleza kuwa tayari eneo hilo limepelekewa umeme wa Kv 33 na TANESCO huku miundombinu ya maji ikiwa inaendelea kuboreshwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.