Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam leo Julai 15, 2022 wametembelea mitambo ya Ruvu Juu na chini inayosukuma maji kupeleka Maeneo mbalimbali ya Mikoa hiyo.
Akiongelea hali ya upatikanaji maji Katika mto Ruvu ambacho ndicho chanzo kikuu kwa Mkoa wa PWANI na Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewahakikishia Wakazi wa Mkoa huo kuwa wameridhishwa na hali ya upatikanaji wa huduma.
Amesema kuwa pamoja na hali ya kiangazi kilichopo sasa, DAWASA imechukua hatua stahiki za kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji msimu wa kiangazi ikiwemo Ujenzi wa Mabwawa ya kutunza Maji.
RC kunenge alihamasiha wanachi kuchukua tahadhari mapema akisema “Tuchukue tahadhari mapema ili kudhibiti upotevu wa maji na tusijikute tunapambana na hali ya mwaka Jana.”
Amesema kuwa hali ya Kina cha maji waliyoikuta kwenye mitambo ya Ruvu juu ni mita 16.5 na Ruvu Chini Mita 4.2 ambapo kwa mujibu wa DAWASA kiwango hicho Kwa sasa kinaweza kutuvusha salama kipindi cha kiangazi.
RC Kunenge amewataka wale wote wenye vibali vya kutumia maji hayo watumie vizuri kwa mujibu wa Vibali vyao na wale ambao wanachepusha maji bila ya vibali waache mara moja ili wasisababishe athari kubwa, na akatoa wito kwa waumini na viongozi wa Dini mbalimbali kufanya maombi na Dua za kuombea mvua za Vuli zinyeshe na bila kusababisha majanga yoyote yale.
Pamoja na hayo kunenge amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za dhati anazofanya kuboresha sekta ya Maji kupitia miradi Mikubwa na midogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameielekeza Kamati ya Ulinzi na usalama na Mamlaka ya Bonde la Wami/Ruvu kufanya Operesheni za Mara kwa mara na kuwachukulia hatua watu watakaobainika kuchepusha maji bila Vibali.
Naye Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kufanya kila jitihada za kuhakikisha kiasi Cha Maji kilichopo kinalindwa na kudhibiti upotevu na akawataka Wananchi kutunza na kulinda Vyanzo vya Maji ili kuwepo na upatikanaji wa maji ya uhakika.
Ziara hiyo pia iliwashirikisha viongozi mbalimbali Katika Mikoa hiyo wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na kamati za ulinzi na usalama.
Mwaka Jana maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam yalikumbwa na tatizo la uhaba wa maji Kutokana na ukame uliosababishwa na kutokunyesha kwa mvua za Vuli.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.