Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amezitaka Halmashauri ambazo zimekuwa zikitoa zawadi hewa kwa watumishi bora wakati wa sherehe za Mei mosi zichukuliwe hatua kalia za kisheria.
Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa sherehe za sikukuu za wafanyakazi duniani kimkoa ambapo risala yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhandisi Martin Ntemo.
Katika lisala hiyo Ndikilo alisema kuwa kuna baadhi ya halmashauri kwenye mkoa huo zimekuwa zikitoa bahasha hewa ambazo hazina kitu licha ya kutangaza kuwa wametoa kiasi fulani kwa watumishi wake bora.
“Hili halikubaliki na wale wanaohusika na masuala haya lazima wachukuliwe hatua kwani hiyo inawakatatisha tamaa wafanyakazi bora kwa kudanganywa kuwa wamelipwa kiasi fulani na mkuu anakabidhi bahasha kumbe haina kitu ni hewa halikubaliki na taarifa za zawadi zilizotolewa zipelekwe kwa RAS ndani ya wiki moja ziwe zimefikishwa,”alisema Ndikilo.
Alisema kuwa wakurugenzi wapeleke michango mbalimbali ya watumishi kwa wakati na kuhusu kuwarudisha wastaafu makwao agizo kwa wakurugenzi walipe kwa wakati na wakae na menejimenti kuangalia madai mbalimbali ambayo ni jambo ambalo limekuwalikijirudia kila wakati hilo lisiwe changamoto kwa mkoa wa Pwani walipe kwa wakati.
“Malipo ya wastaafu hili ni tatizo kubwa sana na kusababisha waingie kwenye mikopo ya moto kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana hivyo ni vema wakalipwa kwa wakati na halmashauri zinazochelewesha hatua zitachukuliwa wakurugenzi wapeleke michango kwa wakati ili wastaafu walipwe mafao yao kwa wakati,”alisema Ndikilo.
Akizungumzia sekta binafsi kutowapatia mikata ya ajira au inamnyima kulipwa stahiki zao hilo limekuwa sugu kwa mkoa huu na kuchafua sifa ya mkoa kuwa unaongoza kwa viwanda rai kwa wadau wa ajira maofisa kazi, mfuko wa wastaafu kwa umma (PSPF), Osha na vyama vya wafanyakazi watatue kwa kufuatilia kujua shida iko wapi.
“Ufuatialiaji wa jambo hilo utaongozwa na ofisa kazi ataratibu hasa kwenye viwanda kwani nini matatizo yanajitokeza hasa anapokuja mgeni mabaraza haya ya wafaynyakazi yako kisheria ambapo taasisi tano zimefanya vizuri na mbazo hazifanyikazi orodha iletwe ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa ndani ya mwezi mmoja na kukata posho za wajumbe wa mabaraza ya kazi ni kinyume cha sheria nataka kujua ili kuchukua hatua,”alisema Ndikilo.
Aidha alitaka vyama vya wafanyakazi visiwe kwa ajili ya mei mosi tu bali wanapaswa kufanya kazi muda wote na washirikiane na viongozi wa mkoa ili washughulikie matatizo ya wafanyakazi na si kusubiri hadi Mei Mosi.
Naye Katibu Tawala mkoa wa Pwani Dk Delphine Magere alisema kuwa kuna tatizo kubwa la mawasiliano baina ya viongozi na wafanyakazi hali ambayo inafanya mambo yasifanyike kwa wakati na maslahi ya wafanyakazi ni changamoto watumishi wanacheleweshewa maslahi yao na haki zingine.
Dk tMagere alisema kuwa changamoto nyingne ni mashauri ya kinidhamu huchelewa hakuna na hakuna sera wala mipango ya mafunzo ikifika kwenda mafunzo baadhi wanakwenda mara kwa mara kwa kujuana baadhi pia wafanyakazi hawajitumi hawafiki kazini kwa wakati wanatoa sababu zisizo za lazima wabadilike na kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii.
Alisema kuwa hatua zilizochukuliwa kwa viongozi wa halmashauri zote walioishi nje ya bajeti na hawakuifuata kuna hatua zitachukuliwa kwani kukiuka sheria ni kosa kisheria barua tumeshapeleke Kisarawe na Kibaha Mji nao watashughulikiwa kila mtu atimize wajibu wake kwa kufuata sheria zilizopo na yaliyo ndani ya uwezo hatua zinachukuliwa na wanaodai madai yao watalipwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.