Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo, ameupongeza mfuko wa kusaidia jamii TASAF kwa kuweza kuwawezesha wananchi wa Mafia ambao waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu.
Hayo ameyasema mwanzoni mwa wiki hii wakati alipotembelea vikundi vya wanufaika wa TASAF kupitia mradi wa kunusuru kaya maskini katika Kijiji cha Changuruma kilichopo katika Wilaya ya Mafia.
Mhandisi Ndikilo alisema kuwa kupitia mradi huu familia nyingi zimeweza kujisimamia na kujikimu kimaisha, ambapo hapo awali zilikuwa haziwezi kuifanya kitu kutokana na hali ngumu za maisha walizokuwa nazo.
“TASAF imerudisha hadhi na heshima ya binadamu, kwani kupitia mradi huu kaya hizi zimeweza kusimama na kusema kwani apo awali familia hizi zilikuwa haziwezi kushiriki katika masuala ya kijamii kwa kuhofia kuchekwa na kudharauliwa”alisema mhandisi Ndikilo.
Pia alisema kuwa kaya maskini ambazo zilizobaki katika mpango huo wa awali bila kuingizwa , zisuburi mpango wa pili zitaziingizwa kama zitakidhi vigezo.
Mhandisi Ndikilo amewataka wanufaika wote wa TASAF wawe na tabia ya kujiwekea akiba na kuweza kubuni miradi midogomidogo pindi mpango huu utakapokwisha waweze kujikimu kimaisha.
“ Rai yangu kwa wanufaika wote wa mardi huu wa TASAF kujifunza kujiwekea akiba ili hapo baadae .TASAF itakapoisha muweze kuanzisha miradi midogo midogo ambayo itawasaidia kujikimu kimaisha na sikutegemea TASAF tu kwani itafika muda itaisha “alibainisha Mhandisi Ndikilo.
Nae Mnufaika mmoja wa TASAF bibi Rehema Mbwana amesema kuwa anaishukuru TASAF kupia mradi huu wa kunusuru kaya maskini kwa kuweza kumsaidia kwani mpaka sasa ameweza kuwasomesha wajukuu zake na kumiliki mifugo.
Katika hatua nyingine mhandisi Ndikilo ametoa jumla ya shilingi laki sita kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkunga katika Zahanati ya Kijiji cha Changuruma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.