Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia majukumu yao ya kikatiba ya Kulinda Raia na Mali Zao Mkoani hapo.
" Ulinzi wenu unatakiwa uwe kwa Raia wote wanyonge, wenye Uchumi wa Kati na matajiri'.
Ndikilo amesema hayo katika hafla ya Jeshi la Polisi Mkoani hapo ya kuaga na kukaribisha Mwaka mpya 2021 iliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Mkoa.
Ndikilo amepongeza jeshi hilo kwa kutekeleza majukumu yake vizuri kwa mwaka 2020, ikiwemo kusimamia ulinzi na usalama wakati uchaguzi, kupambana na madawa ya kulevya, kupambana na uingizwaji wa bidhaa za magendo, kudhibiti ajali barabarani katika barabara ya morogoro(Morogoro Road)
Ndikilo amesema Mkakati wa Mkoa katika kuendele kudhibiti ajali kwenye Barabara ya Morogoro na kuondoa msongamano ni pamoja na Maelekezo aliyoyatoa katika kikao cha Bodi ya Barabara Desemba 2020 ya kukarabati barabara ya zamani ya Morogoro ili itumike pale panapotokea ajali kwenye Barabara ya sasa.
Katika Hotuba yake kwa Hadhara hiyo Ndikilo ameliekekeza Jeshi Jeshi kufanyia kazi mambo Tisa yafuatayo kwa mwaka 2021,
Mosi kulinda Wawekezaji kwa kuwa Mkoa huo ni Mkoa wa Viwanda,
Pili amewataka Jeshi hilo Mkoani hapo kuboresha ushirikiano na kufanya kazi kwa kuelewana na Serikali "Jeshi la Polisi ni Mkono wa kusaidia Serikali kufanya kazi zake" tuongeze kasi ya kushirikiana"
Tatu amelitaka Jeshi hilo kukamilisha Upelelezi kwa Wakati, "Raia wanataka kuona Upelelezi unakamilika na kupeleka mahakamani, "Mahakama haiwezi kuendelea kusikikiza kesi bila Upelelezi kukamilika tunategemeana"
Nne amewataka Jeshi hilo kufanyia kazi migogoro ya ardhi, kwa kufanyia kazi nyaraka ambazo zimeghushiwa."tusiachia baraza la Ardhi pekee" na kukimbia kesi hizi"
Tano amewataka kupambana na kudhibiti Migogoro ya Wakulima na Wafugaji"hatutaki kumwaga damu kwa sababu ya Migogoro hii"
Sita amewataka kuendelea kupambana na Wahamiaji haramu, amewataka kuwashughulikia wale wanaohusika na biashara ya uhamiaji haramu, "shirikianeni na Kamanda wa uhamiaji na wakuu wa Wilaya kulimaliza hili".
Saba amewataka kupambana na Wafugaji wababe, kuna baadhi ya wafugaji ni wababe wanatumia mali zao kunyanyasa wengine.
Nane ametaka Jeshi hilo kufuatilia tuhuma kwenye kata ya Mkange kitongoji cha Java na Matipwili, kwa kuwa kuna biashara za Gongo pombe haramu, ulimaji wa bangi na madawa ya kulevya, ukataji wa Misitu hovyo katika kitongoji cha Java "Mwaka 2021 elekezeni nguvu huko kwani mambo haya yakiendelea yanatupaka matope"
Tisa amewataka Wadau mbalimbali Mkoani hapo kulisaidia Jeshi Polisi kwa hali na mali ili liweze kutekeleze majukumu yake ipasavyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.