• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RC Ndikilo ameridhishwa na Kasi ya Shirika la Umeme Tanesco Mkoa Pwani

Posted on: February 18th, 2021

Kitu Cha kupozea umeme kilichopo Mlandizi ,mkoani Pwani kinatarajia kuongeza uwezo wa upatikanaji wa Umeme MVA 120 ,ifikapo mwezi march mwaka huu na baadae itaongezeka na kufikia MVA 240 kwa mwaka 2022.

Lengo kuu la kuongeza kasi katika upatikanaji wa nishati ya umeme imetokana na mahitaji makubwa ya umeme viwandani na majumbani kutoka 60 mwaka 2015 na kufikia 117.8 mwaka huu.

Hayo yamebainika Februari 17,2021 wakati mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alipokwenda kutembelea kituo hicho ambacho kiliungua na kusababisha changamoto ya upungufu wa umeme ambapo kimefanyiwa maboresho na kuongeza transfoma itakayowashwa mwezi ujao na kuongeza upatikanaji wa umeme wa MVA 120.

Ndikilo alisema, ameridhishwa na kasi ya shirika la umeme Tanesco chini ya meneja mhandisi Mahawa Mkaka ,kutekeleza kwa vitendo mpango mkakati unaoendana na mahitaji ya umeme na hatimae kufikia adhma ya mkoa ya UKANDA wa viwanda .

"Kituo hiki kinapeleka pia umeme maeneo ya viwanda Zegereni kwenye viwanda 25 na majumbani, Bandari kavu ya Kwala na kina hudumia wateja 182,000 kati ya hao ni viwanda vya kati na vikubwa 322 ,hongereni sana 'alieleza Ndikilo .

Aidha,aliitaka Tanesco kushughulikia changamoto ya Mkuranga kuendelea kupata umeme kituo cha umeme Mbagala wakati wilaya hiyo imesheheni kwa viwanda hivyo iondokane na kutegemea umeme katika kituo hicho.

Hata hivyo Ndikilo alielekeza taasisi nyingine wezeshi ya DAWASA na ile inayohusika na barabara kuendana na kasi ya mkoa kuinua sekta ya uwekezaji kwa kufikisha huduma muhimu maeneo ya viwanda .

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji na maboresho ,meneja wa Tanesco mkoani Pwani ,mhandisi Mahawa Mkaka alisema,mwaka 2018-2020 walikuwa wakihudumia viwanda 1,275.

Mkaka alieleza, miradi ya Tanesco kwa mwaka wa fedha 2021-2022 itagharimu bilioni 10.2 kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo na kusogeza huduma ya umeme maeneo 121.


Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.