Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amewasilisha maombi ya uwepo wa huduma za dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Ndikilo aliwasilisha maombi hayo Mjini Kibaha wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa ukarabati wa Sekondari kongwe ya Kibaha na kutembelea Hospitali ya Tumbi kujionea namna shughuli zinazofanywa.
Alisema endapo zitakuwepo huduma za dharura katika Hospitali hiyo itasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na tawi la Mloganzila.
“Hi Hospitali yetu ipo katika barabara kuu ya Chalinze Morogoro ni lango la kuingia na kutokana nchi jirani huduma za kiafya zinatakiwa ziboreshwe sio kukimbiza katika Hospitali ya Muhimbili lakini pia utaratibu wa huduma za dharura ulianza itasaidia wagonjwa wanaotakiwa kwenda Hospitali ya Taifa kuishia hapa hapa" alisema.
Aidha alisema mfumo wa ukusanyaji fedha unaofanywa kwasasa umeongeza mapato kutokana 300,000 kwa siku hadi. Milion 3.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo aliomba kuapitiwa upya gharama wanazotozwa wagonjwa ambao hawakufika hapo kwa kupewa Rufaa.
Kwa mujibu wa moja wa wataalamu wa Hospitali hiyo Radigunda Chuwa alisema kuwa mgonjwa anayefika hapo kwa kupewa rufani kadi yake ni Shilingi 2500 huku aliyefika bila kupata rufani Kati yake akikatiwa kwa Shilingi 5000 ambayo imelalamikiwa na Mbunge huyo kuwa inamuumiza mwananhi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Humphrey Polepole alisema viongozi na watoa huduma wa afya wanatakiwa kutoa Elimu kwa wananchi kuanza kupata huduma za afya kwenye ngazi ya zahanati na vituo vya afya badala ya kukimbilia hospitali za Rufaa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa David Silinde alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila .wananchi anatumia bima ya afya.
Silinde alisema mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo yamepokelewa na yatafanyiwa kazi .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.