MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika kuwa makini kwenye ubadhilifu wa Korosho za wakulima.
Ndikilo amesema asingependa kusikia suala la upotevu wa Korosho kwa kisingizio cha unyaufu na ikibainika hivyo atawashughulikia kukomesha hali hiyo.
Akiongea wakati wa mnada wa kwanza wa Korosho aliouzindua mwanoni mwa wiki hii Wilayani Kibiti Ndikilo alisema kuwa hatafumbia macho kiongozi atakayetajwa kuhusika na wizi huo.
Aidha Ndikilo aliwataka wakulima kuhakikisha wanaanika Korosho zao ikiwa ni pamoja na kuzichambua kuzipanga kulingana na ubora .
Alisema Korosho zisipokuwa katika ubora unaotakiwa wakulima wataendelea kulalamikia soko huku maeneo mengine wakiendelea kuuza Korosho zao katika masoko mbalimbali.
Katika mnada huo wakulima walikubaliana kuuza Korosho daraja la kwanza kwa Shilingi 2153 huku na korosho daraja la pili kuuzwa katika mnada wa pili kutokana na kutoridhika na bei ya mnunuzi ailiyoiweka ya Shilingi 1400.
Said Seif mmoja wa wakulima alisema wakulima hawawezi kukubali kuuza Korosho zao za daraja la pili kwa bei ya Shilingi 1400 ambayo walidai ni ya chini hailingani na gharama wanazotumia wakima hadi Korosho kufika kwenye maghala.
Baada ya makubaliano hayo mkuu wa Mkoa alitoa agizo kwa maofisa ushirika kukaa na viongozi wa vyama vya ushirika kupanga kwa pamoja bei a usafiri hadi kufika kwenye maghala ili zisiwe kubwa zakumuumiza mkulima.
Awali Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji Shangwe Twamala alisema mnada huo ulilenga uuzaji wa kilo 2,073,293 sawa na asilimia 55.9 ya Korosho zote zilizokusanywa na vyama vya ushirika ( AMCOS)
Twamala alisema katika Korosho hizo kilo 512,786 ni daraja la kwanza na kilo 1,560,507.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.