Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, amekabidhi Vifaa na Fedha Taslimu vyenye thamani ya Shilingi 245,867,100 kama Mikopo ya Asilimia10 ya Mapato ya Halmashauri ya Mji Kibaha kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Walemavu.
Akikabidhi vitu hivyo ambavyo ni Pikipiki 12, Bajaji 1, Toyo 1 Mashine 1 ya kutengeneza sabuni na Fedha taslimu shilingi 177,746,400 kwa vikundi 68.
Akizungumza kwenye Hafla hiyo Ndikilo amesema utoaji wa Mikopo hiyo ni Takwa kisheria (Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2019). Aidha ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025.
Aidha alieleza hali ya utoaji Mikopo hiyo na Marejesho Mkoani hapo amesema mwaka 2019/20 Jumla ya Shilingi Bilioni 2.666 zilitolewa kwa vikundi 672 sawa na Asilimia 108 ya fedha zilizopangwa kutolewa na marejesho yalikuwa Sh. 645,770,927 sawa na asilimia 54 ya fedha zilizokopeshwa. "Marejesho haya ni Duni" fedha hizi ni za Serikali lazima mrejeshe ili watanzania wengine wanufaike na matunda ya Serikali yao"
Amesema Kuwa kwa mwaka 2020/21 fedha za asilimia 10 zitakazotengwa na Halmshauri zote 9 ni Bn 2,124,500,000 Hadi Februari 2021 fedha zilizokusanywa ni Bilioni 1,713,172,068 sawa na asilimia 78.54 ya fedha zilizopangwa, fedha ambazo zimefikishwa kwenye vikundi hadi Februari 2021 ni Sh. Bn 1,149,459,447 sawa na asilimia 66.92
Ndikilo Amezitaka Halmashauri zote za Mkoa huo kutenga Asilimia 10 ya mapato ya ndani na kutoa mikopo amewataka kuacha kutumia fedha hizo kwa matumizi mengine.
Pia ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapo kutoa Mkopo hiyo kwa vikundi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria zilizopo. "Tukague vikundi vizuri masharti na katiba zao kabla ya kutoa mikopo"
Amewaasa wananchi na Vikundi wanaopokea Mikopo hiyo kubadilisha maisha yao kiuchumi, ''Ninataka kuona Mikopo hii isaidie kubadilisha maisha yenu kina mama Vijana na watu wenye ulemavu" alisema Ndikilo.
Amewataka kuwa na nidhamu ya Matumizi ya fedha na vifaa wanavyokabidhiwa, "Hakuna fedha ndogo lazima muwe na mipango thabiti ili fedha ziongezeke" alisema Ndikilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.