• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RC Ndikilo awaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa

Posted on: December 18th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, amewaagiza wakuu wa Wilaya Mkoani humo kuhakikisha kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Sekondari unakamilika kabla ya Januari 31, 2018ili  kuwezesha wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba kujiunga na kidato cha kwanza.

Mhandisi Ndikilo  ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa  kikao cha chaguzi za shule kwa wanafunzi kutoka shule za msingi za mkoa wa Pwani waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanaopaswa kujiunga na elimu ya sekondari kidato cha kwanza.

Katika kikao hicho kilichowajumuisha  wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa, Wabunge, wakuu wa shule na wadau wengine wa  elimu  mkoa wa Pwani, Mhandisi Ndikilo ametumia fursa hiyo kueleza kuwa suala  la kukamilisha ujenzi wa vyumba  vya madarasa, matundu ya vyoo na miundo mbinu mingine  katika shule inapaswa kufanywa kwa ushirikiano wa Viongozi  wote na wadau wa elimu ili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari waweze kupata  nafasi.

“Nendeni mkatekeleze maelekezo haya ili  wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika chaguo la kwanza  kutokana  na uhaba wa vyumba vya madarasa waweze kuchaguliwa  na kuanza masomo katika awamu ya pili mwezi Februari” amesisitiza mhandisi ndikilo.

Mhandisi Ndikilo amewataka  wakuu wa Wilaya kwenda kukaa na watendaji wao wanaohusika na maswala ya elimu kutafuta ufumbuzi wa kuzisaidia shule zilizofanya  vibaya kwenye matokeo  ya mitihani ya taifa ya darasa la saba ili kuhakikisha kuwa hazirudii kupata matokea hafifu katika mitihani hiyo ijayo.

Kuhusu kudhibiti suala la mimba kwa wnafunzi mashuleni,  Mhandisi Ndikilo amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuchukua hatua  kwa wale wote  ambao wamewapa mimba wanafunzi na kusababisha wakatishe masomo yao.

“Hakikisheni kuwa wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria “ amesema Mhandisi Ndikilo na kuongeza kuwa “natoa rai kwa  viongozi wa Serikali za mitaa  na watendaji wote kuhakikisha kuwa  yeyote yule atakaejihusisha  na vitendo vya kumaliza kesi za wanafunzi wanaopewa mimba mashuleni kwenye maeneo yao,  nao wakamatwe  na kuchukuliwa hatua kali za kisheria”.

 Mkoa wa Pwani umefanya uchaguzi wa jumla ya wanafunzi 23,270 waliofaulu  masomo ya elimu ya msingi kujiunga na elimu ya sekondari kidato cha kwanza ambapo kati yao wavulana ni 10,835 na wasichana ni 12,335. Ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 66.9 mwaka 2017 hadi kufikia asilia 77.79 mwaka huu na kuuwezesha Mkoa kushika nafasi ya 11 kitaifa.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.