Serikali Mkoani Pwani ,imewaasa wenye viwanda kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya kisheria ya vipimo, ili kumlinda mteja,uchumi wa nchi na kupata tozo stahiki.
Aidha amezitaka ,mamlaka za maji nchini kupeleka mita za maji kupima kwa wakala wa vipimo ili kuondoa malalamiko mbalimbali ikiwemo ubovu wa mita ama matumizi ya maji yasiyoendana na malipo .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati alipotembelea mitambo ya kituo cha upimaji wa Vipimo huko Misugusugu wilayani Kibaha.
“Napenda kutoa rai yangu kwa mammlaka zote za maji nchini wapeleke mita zao kwa wakala wa vipimo ili ziweze kupimwa na pia nawataka wamiliki wa Viwanda kuhakikisha bidhaa wanazozalisha ziwe na vipimo sahihi kulingana na fedha halisi" alisema Mhandisi Ndikilo
Katika hatua nyingine nae ofisa mtendaji mkuu wa wakala wa vipimo ,Dkt Ludovick Manege amesema kituo hicho kinalenga kupima vimimina vya petrol,dizel na mita za maji.
Manege amebainisha , kwasasa wameunda kikosi maalum kwenda kukagua bidhaa viwandani kuangalia kama zinakidhi matakwa ya kisheria ya vipimo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.