Mkoa wa Pwani umepokea jumla ya shilingi Bilioni 4.5 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika Halmashauri za Kibaha Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Kibiti, ambapo kila halmashauri imepatiwa shilingi billioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hizo.
Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Lulanzi Kata ya Picha ya Ndege , kwenye ziara yake inayoendelea ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo. Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kukamilika kwa Hospitali hizo kutaondoa kero ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.
Kila hospitali inatarajiwa kugharimu billioni 1.5 matarajio yetu ni kuona ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa na sio kuanza mradi na kisha kusuasua “alisema Mhandisi Ndikilo.
Aidha, alisema kuwa fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na matumizi yaliyopangwa.
Aidha, Mhandisi Ndikilo aliwaasa Wahandisi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na Serikali ya Mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kutoka Maofisini kwenda kutembelea mradi bila kusubiri ziara za Viongozi ndio watembelee.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo aliwataka wataalam wa mazingira wa Halmashauri ya Mji kibaha kupanda miti katika hospitali hiyo ili kuweka mazingira mazuri katika maeneo ya hospitali hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Assumpter Mshama kwa upande wake alitoa rai kwa jamii kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya elimu na kujitolea kwenye miradi ya maendeleo.
Pia Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege Robert Machumbe alieleza kuwa, nia ya Serikali ni kuwaletea wananchi mabadiliko chanya ya kimaendeleo na amefafanua kwamba eneo hilo itakapojengwa hospitali hiyo ya Wilaya lina ukubwa wa kekari 25.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.