Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wazazi na walezi katika mkoa huo kuacha ubaguzi kwa watoto wao kwa kuwachagulia kazi kwani hakuna kazi maalumu kwa watoto wa kike na kiume.
Alisema kwa kufanya hivyo.ni kuendelea kumbagua mtoto wa kike na kuendeleza mfumo dume kwenye jamii.
Hayo ameyasema leo Mach 8, 2021 katika Kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Ndikilo alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwahamasisha watoto wote bila kubagua jinsia zao kufanya kazi zote kwa bidii lakini pia kuwahamasisha kusoma masomo yote ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwenye maisha yao ya baadae.
Aidha alitoa onyo kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wakike wenye ulemavu Jambo linalosababisha kuwanyima haki zao za msingi.
Aliwasisitisiza wananchi kuwa na ushirikiano katika kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kukomesha vitendo vya mimba za utotoni.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2020 wanafunzi zaidi ya 190 wa Mkoa huo wameshindwa kuendelea na masomo baada ya kupata mimba wakiwa shuleni, ambapo wanafunzi wa shule za msingi ni 39 na Sekondari ni zaidi ya 151. Halmashauri inayoongoza you ni kisarawe ikiwa na wanafunzi 46.
Ndikilo alisema kitendo cha wanafunzi hao kukatisha masomo ni kuendelea kumdidimiza mtoto wa kike.
Alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2020 wanawake 2,316 walifanyiwa vitendo vya ukatili kijinsia ikiwemo kubwaka, kutelekezwa na mimba za utotoni.
Ndikilo ametoa Rai kwa Halmashauri zote Mkoani hapo kutoa fedha za Mikopo za Asilimia 10 ya mapato kwa makundi ya Kinamama Vijana na Walemavu.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa alikabidhi hundi zenye thamani ya jumla ya Shilingi Milion 228 kwa vikundi 26 vya wajasiriamali Wilayani Mkuranga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.