Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe Abubakar Kunengeleo April 25, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Ilse Boshoff Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki na Tanzania wa Kiwanda cha kuzalisha Gypsum board. Kiwanda kwa Tanzania kinapatikana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Mhe Kunenge amemweleza maono ya Serikali ya kukuza Uwekezaji na kuboresha Mazingira ya Biashara, ambapo amemweleza kuwa Serikali inaendelea kuipa kipaumbele Mkoa wa Pwani katika kujenga na kuboresha Miundombinu ya Umeme Maji na Barabara ili kurahisisha Uwekezaji. Aidha amesema Serikali ya Mkoa inaendelea kuvutia Wawekezaji wapya na na kuwa wanaendelea kuhakisha Wawekezaji waliopo wanakuza Uwekezaji wao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Ilse Boshoff amesema amefika kueleleza azma yake ya kuongeza Uwekezaji wao kutoka 15 Million Square hadi 40 Milioni Square. ambapo wakati wote wa upanuzi wa Uwekezaji huo watahitaji Ushirikiano na Serikali ya Mkoa ili kuondoa Changamoto yeyote inaweza kujitokeza.
Kunenge amemhakishia Ushirikiano wakati wa buyujenzi na upanuzi wa kiwanda hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.