Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameshuhudia utiaji wa saini wa mikataba 25 yenye thamani ya zaidi ya sh. Biln 11.6 kati ya Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) mkoa huo na wakandarasi watakaotekeleza miradi hiyo.
Thamani ya mikataba hiyo ya miradi ya ujenzi wa barabara ni sawa na asilimia 37 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo ni zaidi ya Biln 31.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji ameeleza hayo Agost 19 Mjini Kibaha katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Mameneja wa Wilaya hiyo, wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya wakandarasi watakaotekeleza miradi hiyo.
Mhandisi Runji amesema bajeti ya mwaka 2024/2025 vyanzo vya fedha hizo ni kutoka Mfuko wa barabara sh. Biln 7.5, tozo Biln 14.5, Mfuko wa Jimbo Biln 4.5 fedha za miradi ya Maendeleo sh. Milion miatatu na Mfuko wa dharura (kimbunga Hidaya) sh. Biln 1.9.
Akizungumza katika hafla hiyo Kunenge amesema hayuko tayari kuvunja mikataba na mkandarasi atakayekuwa kikwazo katika utekelezaji wa mradi badala yake atamshughulikia katika eneo hilo.
Kunenge amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakapofanya ziara katika Mkoa huo anatakiwa kupokea shukrani kutoka kwa wananchi na sio malalamiko ambayo inasababisha na wanaotekeleza miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakandarasi kufanya kazi zao kwa mujibu wa mikataba huku wakizingatia kwamba Mkoa huo ni wa viwanda na barabara zinatakiwa kuwa imara kurahisisha usafirishaji wa maligjafi na bidhaa kwenda viwandani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri akizungumza kwa niaba ya wakuu wengine wa Wilaya amesema wako tayari kwenda kusimamia miradi hiyo huku akiomba wakandarasi hao kuzingatia ulupaji wa Kodi ambazo zinakwenda kutatua kero za wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Sylvestry Koka amewaomba wakandarasi kutekeleza miradi kulingana na fedha wanazopata Ili ikawe na manufaa kwa wananchi ambao ndio walipa kodi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.