Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wananchi wa Mkoa huo kuacha mara moja tabia ya kuwapokea na kuwahifadhi wageni wasiowajua.
Pia amewataka wananchi hao kuwa waangalifu sana na vipenyo vya kuingia ndani ya Mkoa wa Pwani, ambapo vipenyo hivyo zingi sio rasmi na hutumika kupitisha magendo mbalimbali wakiemo wahamiaji haramu kutoka nchi za Somalia na Ethiopia.
Hayo ameyasema katika kata ya Kisiju Wilayani Mkuranga, katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo alifanya mkutano wa wazi na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.
Mhandisi Ndikilo alisema kuwa mpaka sasa Mkoa umekamata jumla ya wahamiaji 41 ndani ya siku tatu ambao wote ni Raia wa Somali na Ethiopia.
“Wahamiaji haramu ni hatari kwa usalam wa nchi kwani huwezi jua wanakuja kwa shari au kwa wema” alisema Mhandisi Ndikilo.
Pia ametoa rai kwa wananchi wote waliokaribu na fukwe za bahari kusaidia Serikali kwa kutoa taarifa pindi wanapobaini watu hawa.
Mhandisi Ndikilo ametoa maelekezo kwa maafisa Tarafa, watendaji kata na Vijiji kutoa elimuy kwa wananchi kuhusu suala zima la ubaya wa kuhifadhi wahamiaji haramu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.