Serikali Mkoani Pwani, imeagiza wawekezaji wanaohitaji kuwekeza Mkoani humo wahakikishe wananunua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji pamoja na kongani ,ili kuepuka kufanyiwa utapeli na kununua maeneo yaliyo kwenye migogoro ya ardhi.
Aidha halmashauri za mkoa huo zimetakiwa kupima maeneo ya uwekezaji ili kuzirahisishia Taasisi wezeshi ikiwemo Wakala wa barabara mijini na Vijijini (TARURA),Shirika la umeme (TANESCO), Mamlaka ya maji Dar es salaam na Pwani (DAWASA) na Shirika la maendeleo petroleum (TPDC)ziweze kuweka mazingira wezeshi katika mipango yao.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge wakati alipokagua na kutembelea ujenzi wa mradi wa Kiwanda Cha Kinglion Steel kinachojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa zitokokanazo na chuma,huko Zegereni,Kibaha.
"Uwekezaji mkubwa kama huu unahitaji miundombinu yenye gharama,mfano barabara,maji,umeme wa kutosha,gesi ya kutosha, Kwahiyo tuna waambia wawekezaji wetu,vitu hivi ni gharama kubwa.
"
Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi huo, Arnold Christian Lyimo , meneja Kinglion Investment co.ltd ametaja changamoto wanayokabiliana nayo ni uhitaji wa barabara kiwango cha lami km 2 ambayo itasaidia kurahisha usafirishaji wa bidhaa kwenye eneo hilo..
Alieleza, ujenzi huo ulianza march 2022 na utakamilika April 2024 na utaanza uzalishaji Juni 2024 ambapo utagharimu Bilioni 163.
Nae Meneja wa TARURA Mkoani Pwani,Leopold Runji kwa upande wake alisema ,kutokana na changamoto ya barabara kuelekea kiwanda Cha Kinglion wanatarajia kwa kuanza kujenga kwa kiwango cha changarawe kipande kitakachogharimu kiasi Cha sh.milioni 220.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.