• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Serikali Mkoa Pwani yaikabidhi Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake kiucgumi Kampuni ya Go MAMA yenye mtaji na hisa Bilion 50.

Posted on: January 5th, 2023

Serikali Mkoani Pwani,imelikabidhi Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Kampuni Ya GoMAMA yenye mtaji na hisa ya Bilioni 50.

Akitoa rai wakati wa makabidhiano ya majukumu ya Kampuni ya wanawake ya GoMAMA (PLC) kupitia Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoani Pwani,yaliyofanyika Kibaha , Katibu Tawala mkoa wa Pwani,Zuwena Omari alieleza Jukwaa hilo lihakikishe linahamasisha wanawake kuanzia ngazi ya chini ya Vijiji kujiunga na jukwaa pamoja na vikundi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana kwa ajili ya kujiinua kiuchumi.

Aidha alilitaka jukwaa hilo kuanzisha majukwaa mapya katika maeneo ambayo bado hayajaundwa sanjali na kubuni miradi ya uzalishaji .

Zuwena alieleza,Ni wakati wa wanawake wa vijiji, vitongoji nao kujiona ni sehemu ya fursa zinazojitokeza kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Hata hivyo alieleza kwasasa yapo majukwaa yaliyosajiliwa 945 Mkoani hapo ,wajumbe zaidi ya 28,000 ikiwa ni sawa na asilimia 54 .

"Serikali itakuwepo kama ilivyo katika Taasisi nyingine,tutaendelea kuwa washauri kuhakikisha Kampuni inaendelea kung'ara ,sisi Serikali wakati tunashiriki hili suala tulitaka kuona wanawake kwenye vikundi vikiimarika kiuchumi ,nawasihi mkawahamasishe na wenzetu wa chini kujiunga tuone nao wakibadilika kiuchumi na waone ni sehemu ya fursa hizi"

"Kama tumesajili kupata Kampuni hitaji la wanawake kuona wanapiga hatua,asilimia 60 ya umiliki na hisa upo katika majukwaa ya wanawake,hivyo Hawa wenzetu wa hali ya chini tusiwaache nyuma , wanaweza kujiona sio sehemu ya hisa hizi"

Pia Zuwena aliwataka viongozi wa Jukwaa hilo kwenda kutoa elimu ya umuhimu wa Kampuni ya GoMama ,Lengo lake ili wanawake wengi waweze kunufaika.

Akiwasilisha taarifa ya makabidhiano ya uendeshaji wa Kampuni ya GoMama mtaalam mshiriki aliyeratibu mchakato wa uanzishaji Kampuni ya GoMama Mkoani Pwani ,Dr.Ramadhani Mwaiganju alieleza mtaji na hisa ni Bilioni 50.

Alisema ,kila hisa ina thamani ya sh.1,000 ambapo Kampuni itaendeshwa na bodi ya wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano Mkuu.

"Asilimia 60 ya hisa wahamasishwe ziende kwa wanawake wa majukwaa huku asilimia 40 wanahamasishwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwemo wanaume"alifafanua Mwaiganju.

Mwaiganju alitaja malengo ya kampuni kuwa ni kuanzisha biashara zitakazosaidia wanawake kiuchumi na wakala wa kuuza vifungashio kutoka nje ya nchi.

Akishukuru Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwekeshaji Kiuchumi Mkoani Pwani,Mariam Ulega alisema safari haikuwa rahisi na ameshukuru kufikia hatua ya kukabidhiwa Kampuni ya GoMama.

"Namshukuru mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwani yeye ndio muanzilishi wa majukwaa haya, sisi Kama Jukwaa tunataka tuje na mbinu ya kupiga hatua kwa kwenda na Kasi ya mh Rais kwani tumeona akifanya kazi kubwa ya kuifungua nchi ,na sisi tushapewa dira ,nafasi kwa kukabidhiwa kampunii hii ,Tutahakikisha tunatoa elimu ,tutafanya kazi bila kulala"

"Mimi kama Mwenyekiti nitahakikisha Kampuni inasonga mbele ili kumuunga mkono mh.Rais kuhakikisha mwanamke anainuka kiuchumi"alibainisha Mariam.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.