• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Serikali Mkoani Pwani yachukua hatua kuepuka madhara elnino

Posted on: October 19th, 2023

Serikali Mkoani Pwani imeanza kuchukua hatua ya kufanya maandalizi juu ya kuwasaidia wananchi kuepukana na maafa yanayotokana na mvua za Elnino kama ambavyo imetangazwa na mamlaka za Hali ya Hewa nchini ( TMA).

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ameanza kuchukua hatua hiyo leo Oktoba 19 katika Wilaya ya Rufiji Kijiji cha Mohoro Kata ya Mohoro akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Michael Gwimile.

Hatua ambayo tayari imechukuliwa ni pamoja na kuwahamisha wananchi wa Mohoro waliopo kandokando ya Bahari ya Hindi na kuwapeleka kwenye eneo jipya lenye mazingira mazuri ya kuishi hata katika nyakati za mvua.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho, Kunenge amesema kuwa Serikali imeona ianze kujipanga na kudhibiti maafa yanayotokana na mafuriko pindi mvua zinaponyesha kwa kuhakikisha Wananchi wanawekwa katika mazingira salama.

Amesema kuwa wananchi hao wamepewa viwanja bure bila kulipia gharama yoyote na kwamba kila mmoja anapaswa kufanya maandalizi mapema ya kuanzisha makazi katika eneo hilo ambalo litakuwa limeondoa kero ya mafuriko yaliyokuwa yakitokea muda mrefu.

"Leo tumefika hapa kwa ajili ya kufanya maandalizi ya tahadhari juu ya mvua za Elnino ambazo zimekuwa zikileta maafa kwa wananchi wetu na ukizingatia Mkoa wa Pwani umezungukwa na Bahari ya Hindi ambayo imekuwa ikijaa maji wakati wa mvua na hivyo kuleta athari kwa wananchi," amesema.

Ameeleza kuwa Kata ya Mohoro imegawanyika sehemu mbli ambayo ni Mohoro Mashariki na Mohoro Kaskazini na kuna kituo cha afya ambacho mwaka 2021/2022 kilikabiliwa na changamoto ya mafuriko lakini tayari Serikali imelifanyia kazi jambo hilo.

Amesema, eneo walilopata limetolewa na Wakala wa Usimamizi wa Misitu na Mazingira (TFS) ambapo ndani yake kunajengwa huduma zote za jamii ikiwemo kituo cha afya, Shule, Soko, makazi na mahitaji mengine.

Amesema, upatikanaji wa viwanja hivyo umetokana na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye aliyeridhia kugawa eneo hilo kwa wananchi wake na kwamba hakuna budi ya kumshukuru kwa hatua hiyo kubwa.

"Niwaombe wananchi wa Mohoro muungeni mkono Rais Samia kwa hatua hii kubwa aliyoifanya kwa kuhakikisha wote tunahamia katika maeneo tuliyopangiwa , na sisi leo tumekuja kuwahamasisha ili muweze kuhama mapema," amesema.

Amefafanua kuwa mbali na hatua ya kugawa viwanja bure, pia tayari Serikali ipo katika mpango wa kujenga daraja jipya la Mohoro ambalo mara nyingi wakati wa mvua hujaa maji na hivyo kuleta maafa kwa wananchi na wakati mwingine kukosa mawasiliano baina ya pande mbili na akafafanua kuwa tayari usanifu wa ujenzi wa daraja hilo umefanyika na sasa imefikia hatua ya manunuzi na kwamba mkandarasi akipatikana Novemba mwaka huu daraja litaanza kujengwa.

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mohoro Said Hamisi, ameishukuru Serikali kwa hatua kubwa ya kuwahamisha katika eneo hilo na kuwapa viwanja bure ambapo amesema wataitumia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kujenga makazi yao ya kuishi.

Hamisi, amesema katika jambo kubwa ambalo Serikali imefanikiwa ni kuwatengenezea wananchi mazingira mazuri ya kuishi kwani walikuwa wanapata shida kubwa ya kupoteza ndugu zao, watoto na kupoteza mali zao wakati mafuriko yakitokea.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.