Serikali ya watu wa Marekani imekabidhi jengo la kutoa tiba na matunzo ya VVU kwa Zahanati ya Mwendapole Wilayani Kibaha litakalotumika kuboresha utolewaji huduma jumuishi za kinga, tiba na matunzo ya VVU.
Pamoja na jengo hilo, zahanati hiyo pia imekabidhiwa vifaa vya kuzuia na kutibu dalili za awali ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake Mkoa Pwani.
Akizungumza katika makabidhiano hayo ambayo yamefanyika leo Februari 15, 2024, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania Rashid mchatta amesema Serikali ya Watu wa Marekani imekuwa ikifanya kazi kwa Pamoja na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika juhudi za utoaji huduma na kinga, tiba na matunzo kwa watu wenye VVU na UKIMWI katika Mkoa wa Pwani.
Amesema kuwa kutokana na mpango wa Dharura wa Rais wa marekani wa kupambana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia Shirika la US CDC huduma zimefika kila kona ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Pwani.
"Serikali kwa kushirikiana na wenzetu wa US CDC kupitia THPS, imeweka nguvu kubwa sana kwenye mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wale ambao hawajaambukizwa hawaambukizwi, na wale ambao tayari wanaishi na VVU wanapata huduma na matunzo ili waweze kuishi Maisha yao ya kawaida na wasiambukize wengine," amesema Mchatta.
Ameendelea kusema kuwa hadi kufika mwezi Desemba 2023, Mkoa wa Pwani ulikuwa na watu 45,300 wanaopokea huduma katika vituo 85 vinavyohudumiwa na CDC kupitia THPS na akahadhariaha "Kwa bahati mbaya maambukizi mapya bado yapo na ni mengi katika mkoa wetu, wastani wa watu 400 huambukizwa VVU kila mwezi, hii sio taarifa nzuri kabisa, tujitahidi kupambana nayo."
Jengo la kutolea huduma za tiba na matunzo lililokabidhiwa lina thamani ya shilingi milioni 219.0, huku thamani ya vitu vingine vikiwa: samani za Ofisi shilingi milioni 273.6, Vishikwambi 125 kwa ajili ya kusaidia katika huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama Kwenda kwa mtoto (PMTCT) shilingi milioni 90.7, mashine tano za thermocogulation zenye shilingi million 27 na mashine sita za cryotherapy kwa ajili ya matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi zikiwa na thamani ya shilingi million 51.
Akizungumzia hali ya matunzo ya vitu hivyo, Mchatta amewataka watoa huduma za Afya kuzingatia usimamizi bora wa samani zilizoletwa na kuwasisitiza kuwa zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na zitakuwa chini ya usimamizi wa mganga mfawidhi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.