Serikali imetoa kiasi cha shilingi billion 5.653 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo 13 vya afya Mkoani Pwani
Kwa Mujibu wa Mganga mkuu wa Mkoa dk Yudas Ndungile amesema fedha hizo zitatolewa kwa awamu tatu ambapo kwa awamu ya kwanza na Mkoa umepokea kiasi cha Shilingi billion 3.5
Dk Ndungile alisema kuwa awamu ya kwanza kiasi cha billion 1 zimetumika katika kujengea kituochaafya cha Kerege kilichopo Wilayani Bagamoyo nakituo cha Afya Maneromango Wilayani Kisarawe.
Akiwa katika kituo cha Afya cha Kerege Wilayani Bagamoyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikillo alipongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinaongoza Tanzania nzima kwa Ujenzi mzuri na ubora ambao umeendana na thamani ya fedha zilizotolewa.
Aidha Mhe. Ndikiol aliwataka watumishi wa afya kutumia lugha nzuri na staha katika kuwahudumia wanawake wajawazito.
“Kukamilika kwa vituo hivyo kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito ambapo kwa kipindi cha mwaka 2014 wanawake 112 walikufa, na idadi hiyo imepungua hadi kufikia vifo 61 kwa mwaka 2016/2017” alisema Ndikilo.
Pia aliongezea kwa kusema kuwa lengo la Serikali la kutoa fedha hizi ni kutaka kumaliza kabisa tatizo la vifo vya wanawake wakati wa kujifungua, na kukamilika kwa kwa vituo hivi vya afya itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wanawake wanaokwenda kujifungua.
Aidha Mhe. Ndikilo alisema kwamba, Serikali imetoa shilingi million 220 kwa ajili ya vifaa tiba na kuwa baada ya kukamilika kwa vituo hivyo vya afya,vifaa hivyo vitatolewa kwa ajili ya kusaidia wagonjwa husani wanawake wajawazito
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.