Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe Abubakar Kunenge ametembelea na Kukugua shehena hizo zilizokamatwa katika kiwanda cha kutengeneza Alluminium Profile cha LN Features kilichopo Mkuranga.
Akizungumza Baada ya kupokea taarifa ya ukamataji huo Kunenge ameeleza kuwa Mkoa uliunda kikosi kazi kikichohusisha vyombo mbalimbali na Taasisi za Serikali ameongeza kuwa Kikosi kazi hicho kilianza Operesheni hiyo Novemba 21 2024 na kwamba imekuwa na mafanikio kukamata shehena hzo na watuhumiwa mbalimbali ambapo wengine wamefikishwa mahakamani.
Ameeeleza vitu vilivyokamatwa katika Kiwanda hicho ni Shehena za waya za Shirika la Umeme TANESCO, Vipuri vya Miundombinu ya Maji, Vipuri vya Shirika la Simu Tanzania TTCL, vifaa cya miundombinu ya Reli.
Kunenge alieleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya wananchi kuisaliti serikali yao kwa kuhujumu miundombinu inayosambaza huduma muhimu.
“Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha miundombinu, lakini bado wapo wachache wanaohujumu na kurudisha nyuma maendeleo kwa kufanya uharibifu,” alisema Kunenge.
Aliongeza kuwa serikali haitavumilia yeyote atakayehusika katika kurudisha nyuma maendeleo na itafutalia kwa kina kwa yeyote anayehusika na itachukua hatua.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.