Skauti Mkuu wa Tanzania Rashid Mchatta leo Februari 23 ameshiriki maadhimisho ya siku ya mwanzilishi wa Skauti Duniani Baden Powell kwa kupanda miti katika shule ya Sekondari Mwambisi iliyopo mjini Kibaha.
Mchatta ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Pwani amesema zoezi hilo la upandaji miti ni moja ya kazi za Skauti ya utunzaji wa mazingira Duniani na kuwa lengo la skauti kwa Tanzania ni kupanda miti laki tano kati ya hii Fubruari 2024 hadi mwezi April 2024.
"Kaulimbiu ya mwaka huu ni Skauti mmoja mti Mmoja," ameeleza Mchatta na akaupongeza uongozi wa shule ya Sekondari Mwambisi kwa utunzaji bora wa Mazingira.
Katika hatua nyingine Mchatta amewataka wanafunzi kuongeza juhudi katika mafunzo yao ya darasani na Skauti ili kuweza kufikia malengo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.