• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Taarifa ya TANROAD Pwani yawakuna wajumbe Bodi ya Barabara

Posted on: March 7th, 2024

Wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoani Pwani imeandaa na kuwasilisha makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 inayofikia Sh. Bilioni 18.9 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na Sh. bilioni 19.4 Kwa ajili ya maendeleo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji ya matengenezo ya barabara za Mkoa na barabara kuu kwa kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Pwani kilichoketi Machi 7, 2024 kwenye ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Pwani - Kibaha, Meneja wa TANROADS mkoa huo Baraka Mwambage ametaja miradi 18 ya kimkakati inayotekelezwa Mkoani humo ikiwemo ujenzi wa barabara ya mwendo wa haraka (Expressway) yenye Kilomita 220 inayoanzia Kibaha -Chalinze, Daraja la Wami, barabara ya TAMCO - Vikawe (Kilomita 23) na Makurunge -Saadan- Tanga.

Mingine ni Kibiti - Mloka iliyopo Wilayani Kibiti (Kilomita 100.8), Utete - Nyamwage Wilayani Rufiji (Kilomita 33.7), Kibaha - Kisarawe (Kilomita19.8), Maneromango - Vikumburu - Mloka na kuelekea katika mradi wa kufua umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (kilomita 198.71) na Makofia - Mlandizi - Maneromango (kilomita 100).

Kufuatia taarifa hiyo, wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja wametoa kauli ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Meneja TANROADS Mkoa wa Pwani Baraka Mwambage wakisema amekuwa msimamizi mzuri wa miradi ya barabara inayotekelezwa Mkoani humo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Kibiti Twaha Mpembenwe amesema kuwa mhandisi Mwambage amekuwa na ushirikiano mkubwa na hata kutoa ushauri ambao kwa namna moja au nyingine umeleta mafanikio katika Jimbo lake.

Mpembenwe amesema kww sasa anajivunia kuwa na meneja huyo kwani miradi mingi inatekelezeka na sasa Kibiti inafunguka kimaendeleo kwakuwa barabara zinapitika muda wote na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao vizuri.

"Kiukweli meneja huyu lazima tumpongeze kwani anafanyakazi nzuri na amekuwa na ushirikiano mkubwa na mara nyingi amekuwa akitoa ushauri kuhusu fedha zinazotengwa za ujenzi wa barabara kuwa tuzipeleke babaraba fulani huku akitoa sababu ya kwanini fedha hizo zipelekwe huko," amesema Mpembenwe.

Mpembenwe ameongeza kuwa kwa ushauri wa Meneja wa TANROADS na wa TARURA umekuwa ukichochea maendeleo ya Jimbo la Kibiti.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Subira Mgallu amesema kuwa kazi inayofanywa na meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani na meneja wa TARURA Eng. Leopold Runji ni kubwa na inaleta heshima kwa Mkoa wa Pwani.

"Mimi naungana na wenzangu waliotangulia kuchangia katika kikao hiki kiukweli huyu meneja wa TANROADS Mkoa pamoja na meneja wa TARURA wanafanya kazi kubwa na nzuri na sasa hivi tunaona mabadiliko ya barabara ndani ya Mkoa wetu," amesema Mgallu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini Erasto Makala ameunga mkono kauli ya wajumbe wenzake huku akisema barabara nyingi kwasasa zinapitika kutokana na juhudi za meneja wa TANROADS na TARURA.

Makala amesema zipo changamoto ndogondogo za madaraja lakini hata hivyo zinafanyiwa kazi na kwamba matumaini yake baada ya kipindi kifupi Kibaha Vijijini itakuwa na barabara zinazopitika wakati wote.

Katika kikao hicho, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Benard Ghaty amesema kuwa mameneja wamekuwa na ushirikiano mzuri ndio maana chama kinawasaidia kuwasemea pale pesa zinapokosekana za utekelezaji wa miradi husika na akatoa wito kwao kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha zinazokuja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara kwani wakifanya vizuri watakuwa wameleta heshima kwa chama na kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anayepigania maendeleo ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa chama kuipongeza Serikali ni heshima kubwa na kwamba amekishukuru chama kwa msaada wanaotoa na wao wapo tayari kufanya yale yanayokusudiwa kwa heshima ya Rais Samia na Taifa kwa ujumla.

"Sisi wasaidizi wa Rais lazima tuhakikishe tunafanya yale yaliyokusudiwa hasa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwatumikia Wananchi kwa kutatua kero mbalimbali na tukifanya hivyo tutakuwa tumemtendea haki Rais wetu,"amesema Kunenge.Sent from my iPhone

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.