Wakulima zaidi ya elfu 3000 wanaolima zao la mpunga katika bonde la mto Ruvu Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto kwa kipindi kirefu hatimaye wamepata mkombozi baada ya serikali Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kuja na mpango wa kuwaondolea wimbi la umasikini kwa kuwawezesha kiuchimi.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evariost Ndikilo wakati wa halfa ya Makabidhiano ya mkopo matrekta mawili pamoja na pembejeo nyingine za za kilimo zenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 480 kwa kwa uongozi wa chama cha ushirika wa wakulima wa umwagiliaji wa ruvu (CHAURU) ambayo imetolewa na benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB).
“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa kama serikali lazima tujitahidi kw ahali na mali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanawezeshwa kiuchumi na kupatiwa mikopo ya bei nafuu lengo ikiwa ni kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini,”alisema Ndikilo.
Ndikilo alisisitiza kuwa katika kufanikisha azma ya mradi huo mkubwa wa bonde la mto ruvu ataendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha wakulima wote wa mazao mbali mbali ikiwemo mpunga na kuwahimiza wadau wengine wa sekta ya kilimo kuweza kuunga juhudi za serikali katika kuwasaidia wakulima waweze kutimiza malengo waliyojiwekea,
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha wa benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Delick Lugemala ambaye ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuwakomboa wakulima kwa kuwapatia mikopo kwa bei nafuu na kwamba katika Mkoa mzima wa Pwani hadi sasa wameshatoa kiais cha shilingi zaidi ya bilioni 20.
AidhaMkurugenzi huyo alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuendelea kushirikiana na wakulima wa mazo mbali mbali katika kuwasapoti mitaji mbali mbali ya fedha ambayo watakuwa wanaipata kwa liba nafuu lengo ni kuwapatia fursa mbali mbali z akilimo amabzo zitawasaidia katika kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi hivyo benki itaendelea kuwasaidia kwa hali na mali.
Mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika wa wakulima wa umwagilianji Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha amebainisha pembejeo hizo walizozipata na benki ya TADB ikiwemo matreka mawili yataweza kuwaondolea changamoto kubwa za upatikanaji wa zana za kilimo na kuwaondolea hali ya usumbufu waliokuwa wanaupata.
“Kwa kweli Mkuu wa Mkoa tunapenda sana kushukuru msaada huu ambao tumepatiwa kwani hapo awali tulikuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa pembejeo za kilimo hivyo kupelekea baadhi ya wananchama wetu kushindwa kutekeleza majukumu yao ipsasavyo kwa hiyo hii fursa tuliyoipata kwetu ni mkombozi mkubwa kutoka benki ya TADB,”alisema Mwenyekitu huyo.
Pia aliongeza kuwa kutokana na mkopo huo walioupata kutoka benki ya TADB wanachama wake wataweza kupata fursa mbali mbali za kuwezeshwa kupata pembejeo za kilimo kwa wakati na bila ya kuwategemea baadhi ya walanguzi ambao wamekuwa wakiuziwa mchele huo kwa bei ambayo sio rafiki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.