Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji mkoani humo, kupitia kudhibiti rushwa na kupunguza urasimu.
Mhe. Kunenge ametoa pongezi hizo , Januari 24, 2026, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chalinze, iliyopo katika jengo la PCCB House – Chalinze.
Amesema kuwa licha ya uwepo wa miundombinu bora inayovutia uwekezaji katika Mkoa wa Pwani, juhudi za kuhakikisha uwazi, uwajibikaji na mazingira yasiyo na rushwa zimekuwa na mchango mkubwa katika ongezeko la wawekezaji, hali iliyosababisha mkoa huo kuwa na jumla ya viwanda 1,638.
“Nafurahi kuona maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Mkoa wetu. TAKUKURU wamechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha hali hii, kwani katika maeneo yenye rushwa wawekezaji hushindwa kujitokeza kwa wingi,” amesema Mhe. Kunenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.