• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

Tangazeni Miradi ya Serikali : Msigwa

Posted on: May 24th, 2025

Serikali imewataka Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri kote nchini kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu jukumu lao la kuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, wakati wa kufunga kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza katika hafla hiyo, Msigwa alisisitiza kuwa wananchi wanahitaji taarifa sahihi, kwa wakati, na zilizoeleweka kuhusu miradi ya maendeleo, huduma za kijamii, na mikakati mbalimbali ya serikali katika kuwahudumia wananchi.

“Maafisa Habari mnapaswa kuwa sauti ya serikali katika maeneo yenu. Mna wajibu wa kuhakikisha mafanikio ya serikali yanawafikia wananchi, na pia changamoto zinazojitokeza zinaelezwa kwa uhalisia wake,” alisema Msigwa.

Aliongeza kuwa kutowafikishia wananchi taarifa muhimu kunapunguza uelewa na ushiriki wao katika utekelezaji wa sera na mipango ya serikali, hali inayoweza kuchochea upotoshaji au malalamiko yasiyo na msingi.

Serikali, kwa upande wake, imeahidi kuendelea kuwawezesha Maafisa Habari kwa kuwapatia mafunzo, vifaa na teknolojia ya kisasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Msigwa pia amewahimiza Maafisa Habari kushirikiana na vyombo vya habari vya kitaifa na vya jamii ili kuhakikisha taarifa za serikali zinafika kwa wananchi kwa njia mbalimbali.

“Nendeni mkaitangaze serikali – taifa linawategemea nyinyi kama daraja kati ya serikali na wananchi,” alisema Msigwa.



Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Kunenge Ashiriki Kupiga Kura , Awataka Wananchi wa Pwani kuendelea kujitokeza kwa wingi

    October 29, 2025
  • Dumisheni Umoja na Utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu- Kamati ya Amani Pwani

    October 28, 2025
  • Vituo 3,941 vya kupiga kura vyaandaliwa Mkoani Pwani Kuelekea Uchaguzi mkuu

    October 27, 2025
  • RC Kunenge akabidhi Vitendea kazi vya Zaid ya Sh. Bilion 7 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Pwani

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.

  • Situs Toto
  • Situs Slot Gacor
  • AXL777
  • Situs Toto
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • DORA77
  • DORA77
  • DORA77
  • Toto Togel
  • Situs Toto
  • AXL777
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot
  • Toto Slot
  • DORA77
  • KOI200
  • KOI200
  • SILVAWIN
  • AXL777
  • YAMITOTO
  • NABITOTO
  • YAMITOTO
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200