Jumla ya walengwa 30,893 mkoani Pwani wamenufaika na utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) huku zaidi ya sh.bilioni 29 zikiwa zimepokelewa kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi Jan 2019.
Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2018 -2019, katika kikao cha kutathmini shughuli za utekelezaji wa mpango huo, mratibu wa TASAF Mkoani hapa Mratibu wa TASAF wa Mkoa, Asha Itelewe amesema kuwa mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwa walengwa hao.
Aidha ameeleza kuwa wameweza kubadili maisha yao kwani wapo ambao walikuwa wakiishi kwenye nyumba za makuti na sasa wameezeka kuwa na nyumba bora zenye mabati.
Pia maudhurio ya watoto wa kaya hizo mashuleni yamekuwa mazuri kwa Elimu ya msingi na Sekondari pamoja na mlo wa chakula imeongezeka kutoka mlo mmoja hadi milo mitatu kwa siku.
Itelewe ameongeza kuwa ,asilimia 70 ya walengwa wameweza kuanzisha miradi ya kilimo na mifugo na asilimia 50 wameanzisha vikundi vya kiuchumi ili kujiinua kimaendeleo.
Licha ya mafanikio hayo , ametaja changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa raslimali fedha na walengwa kushindwa kujiunga na ya Bima a Afya(CHF) kutokana na kiwango cha kujiunga kupanda kutoka 10,000 hadi 30,000 hivyo wengi wao kushindwa kumudu kiasi hicho.
Nae mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilaya ya Mkuranga Safina Msemo,ameelezea wamejiwekea mkakati wa kuanzisha kilimo cha mapapai ..Msemo anabainisha mkakati mwingine waliojiwekea kiwilaya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.