Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amepokea misaada mbalimbali kutoka Shirika la THPS yenye thamani ya milioni 18 ,kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko katika Wilaya ya Kibiti na Rufiji.
Msaada huo amepokelewa leo April 20 ambapo umekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo la THPS Pro Mohammed Janab.
Akipokea msaada huo Kunenge ameshukuru Shirika hilo,kwa msaada huo na ameahidi kwamba utaenda kuwafikia walengwa kwa muda muafaka.
Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la THP,Profesa Janabi amesema msaada waliotoa ni pamoja na sare za mabegi ya wanafunzi 100, maharage, sukari, unga wa semba ,mafuta ya kula na mchele vyenye thamani ya shilingi milioni 18.
Katika hatua nyingine amempongeza Mh.Rais kwa jitihada kubwa anazofanya kuwasaidia wahanga wa mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini .
Vilevile ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Pwani kwa namna ambavyo unawasaidia waathirika wa mafuriko katika wilaya za Kibiti na Rufiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.