Mkoa wa Pwani umepokea kiasi cha sh bilioni moja zilizotokana na tozo za miamala ya simu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vinne vya afya.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameeleza hayo leo Septemba 10 2021 mbele ya wajumbe wa Kamati ya Siasa Mka waliotembelea Hospitali ya Wilaya ya Kibaha wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo na kujionea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
“Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi hicho cha fedha ili kitumike Kujenga vituo vinne vya afya katika Tarafa zilizopo Wilaya za Rufiji, Kibiti, Mkuranga na Mafia ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za afya katika maeneo yao.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno ameipongeza serikali kwa jitihada za kuboresha upatikanaji wa huduma na kuwaletea wananchi maendele.
“Ninashauri LATRA wafanye haraka kuelekeza magari ya abiria yaweze kufika huku ili kuwarahisishia wananchi wanaokuja kutibiwa kupata usafiri wa gharama nafuu.”
Katika taarifa yake, Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Dr Ibrahim Isack alieleza kuwa hadi sasa ujenzi wa majengo saba ambayo ni ya wagonjwa wa nje (OPD), utawala, wazazi, upasuaji, mionzi, dawa, na la kufulia yamekamilika na kugharimu kiasi cha sh. Bilioni 2.3 na tayari Jumla ya wagonjwa 1436 wameshaudumiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.