Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe: mhandisi Evarist Ndikilo ameitaka Mamlaka ya Mapato Mkoani Pwani kuweka malengo ya kuongeza ukusanyaji wa mapato na kukusanya kwa ufanisi.
"Inatia moyo kama kupitia kikao hiki tungesikia taarifa ya nafasi ambayo tumeshika katika ukusanyaji mapato ukilinganisha na mikoa mingine ya kikodi,Mkoa wetu umekuwa namba ngapi" alihoji Ndikilo.
Hayo ameyasema wakati Akifungua Mkutano wa Jukwaa la Kodi Mkoani Pwani jumamosi Desemba 19,2020 katika Ukumbi wa Ofisi yake.
Ndikilo ameitaka Mamlaka hiyo (TRA )Pwani kuwasilisha Takwimu za kuongezeka au kupungua kwa walipa Kodi. "Kupitia kikao hiki tungejua ulipaji Kodi unaongezeka au unapungua" Ameitaka pia kuwasilisha Takwimu na Orodha za namba za walipa kodi (TIN) za wanaofanyabiashara Pwani zilizohamishiwa Pwani kutoka mikoa mingine, "ni lazima wale wanaofanya Shughuli zao katika ardhi ya Pwani kulipia kodi Pwani" alisisitiza Ndikilo. Aidha ameitaka kuwasilisha orodha za walipa kodi ambao hawajahamisha TIN zao ili kufanyia kazi pale anapowatembelea.
Ameeleza kua kupitia takwimu hizo Mkoa ungejua utekelezaji wa maagizo yake ya kuhamishia TIN Pwani katika kuongeza makusanyo, inafurahisha kama leo katika kikao hiki tungepata taarifa hii alisema Ndikilo.
Akizungumzia kuhusu upanuzi wa Wigo wa Kodi Mkoani hapo Ndikilo ameitaka TRA kujipanga kwa ukusanyaji wa mapato kwenye eneo jipya la Kwala ambapo Mkoa umeomba kapewa ekari 4000 kwa ajili ya Shughuli za uwekezaji na Ujenzi Viwanda, ameongeza kuwa Mamlaka hiyo iangalie sasa Wilaya ya Mafia ambapo tayari kutakuwa na kivuko na hivyo kutaongeza Shughuli za uchumi,
Ametaja pia Ujenzi wa wa barabara mbili za Lami za TAMCO Mapinga na Makofia Mlandizi zitakazo unganisha wilaya zetu na Mkoa wa Dar es salaam vyote hivi vitahamasisha Shughuli za kiuchumi na hivyo ukusanyaji mapato Alisema Ndikilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.