Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amesema hatovumilia juhudi zozote zinazo hujumu agenda ya Ujenzi wa Viwanda Mkoani humo, ameyasema hayo Desemba 17,2020 wakati alipotembelea Plot Na. 57 inayomilikiwa na Kampuni ya Saibaba na Plot Na. 55 yenye Ujenzi wa Kiwanda cha vifaa vya Plastiki cha Kampuni ya Weixing plastic Cement Ltd vilivyopo picha ya Ndege Kibaha.
Akijibu Kero ya Kampuni ya Weixing ya kutakiwa kubomoa ukuta na kulipa Usd 25,000 kwa Kampuni ya Saibaba anayepakana naye Ndikilo amesema jambo hilo halikubaliki. Ameeleza pingamizi hizo zinakwamisha ujenzi wa Kiwanda hiki cha Kampuni ya Weixing na ni kukwamisha pia juhudi za Serikali za kuvutia uwekezaji katika ujenzi wa viwanda,
"Kinachofanywa na Saibaba ni kukwamisha juhudu za Serikali za ujenzi wa viwanda kwa kuleta pingamizi na visa kitu ambacho kama Mkuu wa Mkoa sitakikubali"
"Hatuwezi kukubaliana na mambo ambayo yanahujumu ujenzi wa viwanda" alisisitiza Ndikilo
" Saibaba anamiaka 5 sasa hajaendeleza eneo hili, Kampuni Weixing ndani ya miezi saba tangu apate ardhi kaanza Ujenzi na kaleta Ajira100, na ifikapo Januari wataanza kuzalisha na kutoa ajira 300, lazima tutengeneze mazingira mazuri kwa kampuni hii ili tupate kodi, na ajira" alisema Ndikilo
"Mwekezaji huyu Weixing ameniongezea kiwanda kwenye orodha ya viwanda vyetu ndani ya Mkoa" alisema Ndikilo.
Pingamizi hizi za Saibaba zimekuja baada ya kukosa biashara ya kumuuzia kiwanja Kampuni ya Weixing.
Ndikilo amewataka Wawekezaji hao kupendana na kulinda uwekezaji wao, "muache uhasama kwa kuwa kila mmoja anamuhitaji mwingine, mkikaa kama maadui hamsalimiani ni mbaya, mtashirikiana kwenye mambo mengi Moto, wizi nk.
Hizi kelele na pingamizi zikome mara moja, zikiendelea zitakwamisha uwekezaji huu" alisema Ndikilo.
Ameitaka Kampuni ya Saibaba kufika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kuwasilisha changamoto na Ofisi yake itamsikiliza na kumuunguniaha na taasisi zinazohusika.
Amezitaka kampuni hizo mbili pale ambapo wanachangamoto wakae mezani na kumaliza tofauti zao
"Wawekezaji ni watu wa muhimu katika Mkoa wetu tunakaa nao mezani tunawasikiliza na kutatua changamoto zao milango yetu ipo wazi masaa yote kwa ajili yenu" alisema Ndikilo
Ameitaka Kampuni ya Weixing kuwalipa wafanyakazi wake vizuri na kupanga namna ya kuchangia jamii inayoizunguka kupitia .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.