WAZIRI wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema ukuaji katika sekta ya uwekezaji umetokana na juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza nchi kwenye mataifa mbalimbali.
Ameyasema hayo Dec 20 wakatai alipokuwa akifunga maonyesho ya nne ya biashara na uwekezaji yaliyofanyika Mjini Kibaha Mkoani Pwani ambayo yamehusisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa viwandani.
Ulega amemshukuru Rais kwa kufungua uchumi hapa nchini ambapo kumekuwa na uwekezaji mkubwa unaendelea katika maeneo mbalimbali huku Mkoa wa Pwani ukiongoza kwa kuwa na wawekezaji wengi.
Amesema kutokana na kile kilichofanywa na Serikali ya awamu ya sita kumesababisha ongezeko la mitaji ambayo imefikia dola za kinarekani 42.1 jambo ambalo linazidi kuinua uchumi.
Pia amewataka watanzania kuhakikisha wanafika kipaumbele Cha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwani wawekezaji wengi wamekuwa wakitumia malighafi za ndani ya nchi.
Akizungumzia kuhusiana na Changamoto kwenye baadhi ya sekta amesema Serikali inaendelea na kutatua vikwazo vilivyopo na kwamba maboresho kwenye barabara yataendelwa kufanyika Ili ziweze kupitika muda wote.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ameeleza kuwa tatizo la umeme katika mkoa huo linashughulikiwa kwa ufanisi kupitia ujenzi wa transfoma kubwa ya MVA 120 inayoendelea kujengwa katika eneo la Mbagala. Transfoma hii inatarajiwa kusaidia kusambaza umeme katika maeneo ya Mkuranga.
Aidha, mfumo wa umeme wa KV 400 utatoka kwenye substation ya Chalinze na utaunganisha maeneo mbalimbali, ukiwemo Chalinze hadi Kinyerezi, huku mfumo mwingine wa KV 220 ukikusudiwa kusambaza umeme maeneo ya Bagamoyo.
Kunenge amesema kuwa mradi huu utasaidia kumaliza changamoto za upungufu wa umeme, na kusababisha upatikanaji wa umeme wa kutosha katika mkoa wa Pwani.
Hii pia inatarajiwa kuwafaidi wawekezaji kwa kuwa sasa watapata umeme wa uhakika na hivyo kuwawezesha kuzalisha muda wote.
Pia ameomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuwajengea Bomba la gesi ambalo litawafikia wawekezaji wa viwandani wenye uhitaji wa kutumia gesi.
Kwa upande wa washiriki wa maonesho hayo wameushukuru mkoa wa pwani kwa kuandaa maonesho hayo kwani yamewapa fursa kukutana na wateja wengi na kutangaza bidhaa zao pamoja na kubadilishana uzoefu baina ya wafanyabiashara.
“Nashukuru uwepo wa maonyesho hayo kwani yamenipa fursa ya kukutana na wateja wengi na kutangaza bidhaa zangu pamoja na kubadilishana uzoefu na wajasilimali wenzangu pia” lisema Afisa Masoko wa Kiwanda cha Dowercare Technology Lucia Msami.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu amesema uwepo wa maonyesho hayo umekuwa fursa kwao kutoa elimu kwa wananchi wengi walipotembelea Banda lao lililokuwa likitoa huduma muda wote wa maonyesho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.