Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutembea kifua mbele kutokana na yale yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Taifa hili.
Akizungumza kwenye kikao kazi na Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Mary Chatanda, Kunenge alisema hiki ni kipindi chao kutamba kutokana na utendaji wa hali ya juu unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa pekee katika dunia hii kutokana ushawishi wake mkubwa ambao amekuwa akiufanya kwenye mataifa mbalimbali,” alisema Kunenge.
Aidha amewapongeza viongozi wa UWT Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Mary Chatanda amempongeza RC Kunenge kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika chama na akasema kuwa hiyo ndio sahihi katika utendaji shirikishi kati ya chama na serikali tunaouhitaji.
Aidha Bi. Chatanda amemtaka Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa miongoni mwa watekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi kwa usimamizi uliotukuka wa miradi ya maendeleo kwa jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.