Mrajisi mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini Tito Haule, amewaagiza viongozi wa vyama vya ushirika mkoani Pwani kuweka msukumo zaidi wa kusimamia vyama vyao ili viweze kujiendesha na kuleta tija kwa Wananchi.
Akizungumza katika jukwaa la Ushirika mkoani Pwani, Haule amesema tatizo la Vyama vya ushirika kushindwa kujiendesha kwa faida kunatokana na udhaifu uliopo kwa baadhi ya viongozi ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia vibaya nyadhifa zao na kuhujumu mali za ushirika.
Pia amewataka viongozi hao kuwa waadilifu katika kusimamia mali za ushirika na kamwe wasikubali kuwachagua viongozi ambao hawataweza kusaidia kuimarisha vyama vyao.
Nae Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa Mkoa wa Pwani Anjela Nalimi amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa maafisa ushirika pamoja na vitendeakazi jambo ambalo linafanya washindwe kusimamia ipasavyo vyama vya ushirika vilivyoko katika maeneo ya vijijini”.
“Mkoa wa Pwani unajumla ya vyama vya ushirika 613, ambapo kati ya hivyo vyama vinavyofanya kazi ni 245 tu,”alisema Nalimi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.