Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuleta maendeleo mkoani humo, hususan katika sekta ya viwanda.
Kunenge amesema tangu Rais Samia aingie madarakani mwaka 2021, idadi ya viwanda mkoani Pwani imeongezeka kutoka 1,387 hadi kufikia 1,681. Kati ya hivyo, viwanda vikubwa vimeongezeka kutoka 59 hadi 97, sawa na ongezeko la asilimia 73, huku viwanda vya kati vikiimarika kwa viwanda 71 zaidi.
Aidha, amesema ongezeko hilo limechangia upatikanaji wa ajira zaidi ya 21,000 za moja kwa moja na zaidi ya 60,000 za muda mfupi. Hivi sasa mkoa huo una viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo televisheni, nondo, vioo, magari, saruji, chuma, pamoja na dawa za mifugo na binadamu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.