Raia wawili wa kigeni wamekamatwa wakiishi katika eneo la Mapinga Kibosha Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kinyume cha sheria za nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya usalama mkoa huo Alhaj Abubakari Kunenge amewataja Wawili hao kuwa ni Livingston Ese Onayomake raia wa Nigeria na Bertrand Noubissie wa Cameroon.
Kunenge alieleza kuwa Mcameroon Noubissie alikutwa na karatasi zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchapisha noti bandia, kemikali na kasiki la kutunzia fedha huku Ese Onayomake raia wa Nigeria akikutwa na paspoti 34 ambazo si za kwake, ambapo kati ya hizo paspoti 32 ni za Nigeria na paspoti mbili zikiwa ni za Ghana.
"Huyu raia wa Nigeria alipohojiwa, alidai kuwa alichukua pasipoti hizo
kwa lengo la kuwatafutia wahuskia viza ya Uturuki," alisema Kunenge.
Mkuu huyo wa Mkoa alionya kuwa hatomvumilia raia yeyote wa nje atakaetaka kuishi Mkoani humo kinyume na Utaratibu ambapo ameeleza wale wanaoishi bila kufuata sheria na kubainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Nae afisa uhamiaji mkoa wa Pwani, Omary Hassan alieleza kuwa walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupokea taarifa fiche Februari 9, 2023 wezi kutoka kwa msiri wao akieleza kwamba katika eneo tajwa kuna watu ambao uraia na mienendo yao yanatia shaka na Februari 10 timu ya Maafisa Uhamiaji walifanikiwa kufika katika eneo husika na kutekeleza jukumu lao ambapo walikamata raia hao wawili wa Afrika Magharibi na kuwafanyia upekuzi maungoni na kwenye makazi yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.