Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kufuata moyo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na kwamba kufanya hivyo ni ibada.
Mhe. Kunenge ameyasema hayo leo Disemba 23, 2022 wakati akikabidhi msaada wa vyakula vilivyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Madina, Vikawe Halmashauri ya Kibaha Mji Mkoani Pwani.
Vyakula vilivyokabidhiwa ni mchele, mbuzi wawili, maharage, viungo na mafuta.
Mhe. Kunenge amesema Dkt. Samia ni Rais wa nchi lakini hakuangalia nafasi ya madaraka aliyonayo na kuguswa kuwasaidia watoto yatima kwa kuwapatia msaada wa vyakula ili washiriki na watoto wengine duniani kusheherekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.
"Nitoe wito kwa wakazi wa mkoa wa Pwani, watoto hawa ni wakwetu hivyo tunajukumu la kuwasaidia," alisema Mhe. Kunenge.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto katika kituo cha watoto yatima cha Madina Fatuma Salum, pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamemshukuru Rais Dkt. Samia kwa msaada huo na kwamba amewafanya kuwa wenye furaha kama ilivyo kwa watoto wenye wazazi.
kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya kibaha mwalimu mwajuma Nyamka aliyemwakilisha mwenyekiti wa CCM mkoa wa pwani Mwinshehe Mlao amesema licha ya kwamba rais Dkt. Samia amefanya ibada kwa kuwasaidia watoto yatima lakini pia ametekeleza ilani ya chama hicho iliyoanisha kuyasaidia makundi hayo.
Rais Dkt. Samia amekuwa akitoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima na wanaolelewa katika vituo mbalimbali vilivyopo katika mikoa yote hapa nchini Kila mwaka hususani wakati wa sikukuu za kidini na za kufunga mwaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.