Jumla ya kilo 5,623,277 za korosho zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 16. 324 tayari zimelipwa kwa wakulima Mkoani Pwani.
Aidha Wakulima wa Korosho 24,543, wenye kilo 14,370,844 kati ya kilo 21,130, 598 zilizopo kwemye Maghala makuu wameshahakikiwa sawa na asilimia 68.
Hayo yamesemwa Wilayani Mkuranga na Rufiji wakati na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipo kuwa kwenye ziara yake katika Wilaya hizo.
Alisem a zoezi la uhakiki ilikuwa mwisho Februari 15 lakini Mkoa wa Pwani umeomba kuongezewa muda hadi rerbruari 28 mwaka huu, kwa kuwa umechelewa kuanza zoezi hilo kutokana na chagamoto mbalimbali ikiwapo kuchelewa kwa kutolewa kwa bai ya korosho daraja la 11 ambapo ilielekezwa kuwa bei hiyo ni asilimia themanini ya bei ya korosho Daraja la Kwanza.
Mhandisi Ndikilo aslise kuwa , Korosho zilizokusanywa mwaka huu ni kilo 23,066,238 ambapo kilo 21,130,598, sawa na asilimia 91.6 zipo kwenye Maghala makuu
“Ghala kuu la Mwanambaya zipo kilo 6,549,204, Kibiti kilo 2,650,529, TANITA kilo 1,705,621, kurasini SCALABLE kilo 6,325,237, Kiegeani –Mafia kilo 213,593 na kilo 6,488,690 zipo kwenyew Maghala madogo ya AMCOS”alisema Mhandisi Ndikilo.
Nae pia Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, Shangwe Twamala alisema kuwa Mkoa wa Pwani ulichelewa kuanza ukusanyaji wa Korosho, kwani ukusanyaji huo ulianza Oktoba 30,2018 tofauti na Mikoa ya Lindi ,Mtwara na Ruvuma ambayo yenyewe ilianza mapema.
“Baadhi ya Korosho kuwepo kwenye Maghala ya AMCOS ni changamoto kubwa sana, sasa ili kutatua changamoto hii tunashauri malipo kwa wasafirishaji yafanyike kwa wakati ili waweze kufanya kazi hii”
“Kama itawezekana tutumie magari ya jeshi kuhamisha Korosho kutoka kwenye AMCOS kwenda Kwenye Maghala ya kurasini” alieleza Twamala.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema kuwa zaid ya tani 4,000 za korosho kati ya 6,000 walizokusanya zipo chini ya sakafu ambapo wamezitandikia maturubai lakini wanahofia unyevu unyevu zisije kuharibika.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo kwa upande wake alisema kuwa, wakulima Wilayani hapo wamelipwa korosho sh. Bilioni 3.7 kwa wakulima 2,665.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.