Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi kwenye viwanda kusoma sheria za kazi za hapa nchini na za wawekezaji ili inapotokea tatizo wajue sehemu sahihi ya kufikisha matatizo yao.
Mhe. Samia aliyasema hayo wakati alipokua Mkuranga katika ziara yake ya kikazi ya siku sita kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri za wilaya ya Kisarawe, Mkuranga, Kibaha na Bagamoyo pamoja na kuongea na wananchi.
Alisema, wafanyakazi viwandani wanatakiwa kujua sheria iliwanapoona kuna tatizo kwenye maeneo yao ya kazi wajue sehemu ya kwenda kuyafikisha yapatiwe ufumbuzi.
Akiwa katika katika kiwanda cha gypsum cha KNAUF aliwataka wananchi kulinda viwanda vilivyopo ili viweze kuwanufaisha wananchi kwa kupata ajira.
Alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwajali wanafunzi tofauti na wawekezaji wengine ambao wanaangalia zaidi maslahi na faida kwenye viwanda vyao.
Aidha akiwa katika kiwanda cha vigae kilichopo Mkiu aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili wawekezaji waendelee kuongezeka kuwekeza hapa nchini.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo alisema wilaya ya Mkuranga ina viwanda 61 vikubwa ambapo aliwataka wadau kutumia gesi asilia.
Mkurugenzi wa kiwanda cha KNUF Geogious Zachopolous alisema mapato yanayopatikana katika kiwanda hicho wananufaika pamoja na wananchi katika shughuli za kijamii.
Mkurugenzi huyo alisema wataendelea kushirikiana na serikali katika uwekezaji kutatua changamoto za ajira kwa vijana ikiwa na kuwafundisha ujuzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.