Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Mchatta, amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Mgawa, Wilaya ya Mkuranga, kwa mchango wao mkubwa katika ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji hicho.
Mchatta alitoa pongezi hizo leo alipokuwa akikagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, baada ya uzinduzi wake tarehe 2 Aprili 2025 katika Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani.
Wananchi wa kijiji hicho wamechangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa shule hiyo, ikiwa ni shilingi milioni 49.254, huku Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ikichangia asilimia 60 ya gharama kupitia mapato yake ya ndani. Ujenzi wa shule hiyo unatarajiwa kumaliza changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.