Wanawake wa mkoa wa Pwani wameaswa kutumia vyema fursa zinazotolewa na serikali kukuzia uchumi wa familia zao.
Hayo yamesewa na mbunge wa viti maalum wa mkoa huo Subira Mgalu kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya shule ya msingi Mtongani wilayani Kibaha.
Nia ya serikali ni kuona wanawake wote wanawezeshwa ili kuwa na mitaji itakayowasaidia kuanzisha miradi midogo midogo itakayowapatia kipato na kuwaondoa katika hali ya utegemezi," amesema.
Naye mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Pwani dokta Alice Kaijage amewasihi wanawake wa mkoa huo kuwekeza kwenye kutoa elimu kwa watoto wa kike na malezi bora kwa familia zao.
Akiwasilisha salam za mkuu wa mkoa wa PWANI Abubakari Kunenge, mkuu wa wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri ameiomba jamii iendelee kushrikiana na serikali kupiga vita vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.