Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe. Abubakar kunenge, Juni 14, 2021 ameshiriki kikao Maalumu cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani kupitia na Kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mwaka 2019/2020 Wilayani Mafia.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mhe.Kunenge ametumia wasaa huo kuwapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kupata hati safi. Amewataka kufunga hoja za ukaguzi kabla hazijafika kwenye hatua ya kutakiwa kujieleza ili kuepuka kuzalisha hoja zaidi.
Amemtaka Mkurugenzi na Vyombo vya Dola Wilayani hapo kuanza uchunguzi na kuchukua hatua kwa watumiaji (Watumishi) wote ambao wametumika kuzalisha hoja. Amewataka watumishi kufuata utaratibu, kuheshimu sheria na kuwasilisha nyaraka katika Matumizi yote ya Fedha ili kuepuka kuzalisha Hoja.
"Sitopenda kuona hoja zinaongezeka na kujirudia kwa mwaka ujao" alisema Kunenge
Ameitaka Halmashauri hiyo kubuni vyanzo vipya vya mapato kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi.
Amewataka pia Viongozi wote wa Nafasi za Kisiasa na Kitaalamu Wilayani hapo kushirikiana katika kutekeleza Majukumu yao, "Wafanya maamuzi pokeeni ushauri wa Wataalam ili mfanye maamuzi sahihi" amesema Kunenge.
Amewaeleza amekuja kufanya kazi Mkoa wa Pwani, na kuwataka Wataalamu wote Mkoani hapo kuandaa Taarifa yenye Fursa zote Muhimu katika sekta zilizopo Mkoani hapo ikiwemo vyanzo vya Mapato, Huduma za Kijamii, Viwanda Kilimo, Biashara, Utalii, Uvivu ili kupata hali ilivyo kwa sasa na kuainisha maeneo yote yanayohitaji maboresho.
Ameeleza kupitia Taarifa hiyo watakuwa na Siasa nzuri ya Kiuchumi ya kutumia kidogo kupata kingi, Ameeleza kuwa kufanyia Kazi vipaumbele hivyo muhimu na kuvifanyia kazi kutaleta maendeleo ya haraka ya Wilaya na Mkoa huo.
Mhe. Kunenge ameeleza kuwa ili kuleta maendeleo ya haraka ya Mafia ni lazima Viongozi na Wafanyakazi Wilayani hapo kuondokana na dhana ya Mafia ni eneo la pembezoni lenye shida, amewataka kuanza kunadi upya Wilaya ya Mafia.
Kuhusu Changamoto ya uhaba wa watumishi, Taa kwenye Kiwanja cha Ndege, Tozo za magari mara mbili kwenye Bandari ya Nyamisati na Kilindoni mafia amesema ameyachukua na atayafanyia kazi.
Pamoja na mambo mengine Akiwa Wilayani hapo Mhe. Kunenge amepokea Taarifa ya Wilaya, kuzungumza na Baraza la Madiwani na Kutembelea Kiwanda kikubwa cha kuchakata Samaki cha TANPESCA Ltd.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.