Watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani wameaswa kutumia lugha nzuri, katika kutoa huduma kwa Wananchi na kufanya kazi kwa bidii bila ya upendeleo wa aina yeyote.
Rai hiyo ilitolewa leo na Katibu Tawala Mkoa Pwani Bi Theresia Mmbando wakati wa mkutano wa kazi baina yake na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani, ambapo katika mkutano huo pia alichukua nafasi ya kujitambusha kwa watumishi hao.
Aidha Bi Theresia aliwataka watumishi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao na kumpa ushirikiano wa kutosha katika kuwahudumia wananchi kwa wepesi na weledi.
Pia aliwataka watumishi hao kuwahi kazini ili kuweza kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa wakati na kuwasisitiza kuwa ni lazima kila mtumishi afuate maadili na kanuni za Utumishi wa Umma .
Bi Theresia Mmbando amechukua nafasi ya Ndugu Zuberi Samataba aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.